GAMBO AWATAKA MADEREVA BODABODA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUFICHUA UHALIFU MKOANI HUMO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 15 March 2020

GAMBO AWATAKA MADEREVA BODABODA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUFICHUA UHALIFU MKOANI HUMO


Sehemu wa Madereva bodaboda wa Mkoa wa Arusha wakiwa kwenye mkutano wao na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwenye ukumbi wa Hotel ya Mount Meru jijini hapa picha na Ahmed Mahmoud Arusha


Na Ahmed Mahmoud Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha  Mrisho Gambo ameliamuru  Jeshi la polisi kuziachilia Pikikipi zote Zenye makosa madogo madogo yasiyohusiana na mtukio ya  uhalifu zilizoshikwa kwenye Vituo vya polisi .

Ametoa Agizo hilo wakati wakikao chake chakutatua changamoto zinazowakabili madereva wa bodaboda Mkoa wa Arusha Takribani 1000 wakiongozwa na viongozi wa umoja huo ikiwemo Uboja na Uwapa.

Gambo amesema kipaumbele cha kwanza ni usalama wa wananchi ndani ya Mkoa, na haridhishwi na askari wanaokamata pikipiki zenye makosa madogo yanayotatulika na kuziandikia faini zinazoendana na magari makubwa uku kipato chao nikidogo nakuagiza kuachiliwa kuanzia sasa na maderava kuzifuata pikipiki zao.

Pia ameongeza kuwa wanapojenga hoja juu ya maslahi na maendeleao kwa madereva hao,nakuwataka kutokutumika kisiasa kwani viongozi wengi  huwatumia kwa manufaa yao uku serikali ikijipanga kuhakikisha wanamaliza kero na shida zao.

" nataka viongozi na watendaji ndani ya serikali wajali kero na shida za wananchi wanyonge la sivyo wakae pembeni kwani kipaumbele cha Mkoa nikariba ya  viongozi wanaoshughulikia shida za Mwananchi.

Katika hatua nyingine Gambo amewataka viongozi wa vijiwe kuandaa utaratibu mzuri wa kuchangishana Fedha kwaajili ya kuwa na mfuko wa  Maendeleo wakusaidiana pindi ikitokea mtu anakodisha pikipiki anunuliwe nakumtaka Rpc kufuatilia Fedha zilizochangwa zipo wapi,nazimefanya nini

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana alisema wamelipokea agizo hilo nawanakwenda kulifanyia kazi kuanzi Leo.

Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha Merry Kipesha Amesema bodaboda wanapaswa  kutambua hiyo nikazi yenye staha na serikali imehalalisha kuwa rasmi hivyo kufuata sheria bila shuruti nakuwa sehemu yakutoa ushirikiano kwa serikali  kuondoa uhalifu na makosa ya barabarani.

Baadhi ya maderava bodaboda wamesema mpaka sasa uongozi uliopo umekuwa ukiwanyanyasa kwa kupatia makosa jambo ambalo wameomba kufayika utaratibu wakuchagua viongozi watakaojali maslahi na kuwatetea.

Uku wakiomba taarifa fiche pindi wanapotoa Taarifa za kiuhalifu kwani imekuwa ikihatarisha maisha yao pindi wahalifu wanapotoka.

No comments:

Post a Comment