KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 15 March 2020

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Mwenyekiti wa Kamati akipanda mti wa matunda kama kumbukumbu.

Muonekano wa baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Halmashauri ya Mbulu.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Mwita Waitara akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji Hudson Kamoga.

Naibu Waziri Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Mary Mwanjelwa akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji Hudson Kamoga.

Mbunge wa Manyoni Mashariki Mhe Daniel Mtuka(aliyeshika simu), Mbunge wa jimbo la Kilolo Mhe Venance Mwamoto(wa tatu kutoka kushoto), Mbunge wa jimbo la Kyerwa Mhe Innocent Bilakwate(wa pili kutoka kulia) pamoja na watumishi wa Halmashauri.

Mkurugenzi Mtendaji Hudson Kamoga akisoma taarifa ya Ukenzi wa Hospital ya Wilaya mbele ya Kamati.

Mwenyekiti wa Kamati Dkt Jason Rweikiza na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga na kamati wakati wa ukaguzi.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, imefanya ukaguzi na kuridhishwa na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, inayojengwa katika kata ya Dongobesh wilayani Mbulu.

 Akieleza kuridhishwa kwake na hatua ya ujenzi na matumizi sahihi ya fedha za Serikali, Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt, Jason Rweikiza amesema Kamati ya Bunge imeridhishwa na hatua ya ujenzi kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali, na kuitaka Ofisi ya Rais TAMISEMI, kuhakikisha fedha zilizotengwa kwenye bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya Hospitali hiyo zinatolewa haraka ili kukamilisha miundombinu iliyobaki ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyokusudiwa.

 Kwa upande mwingine, Kamati imempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga na timu yake yote ya wataalam kwa usimamizi mzuri na kumtaka kuhakikisha anasimamia kikamilifu ukamilishaji wa Hospitali hiyo mara fedha zitakapoingia.

 Wakati huo huo Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara ameihakikishia Kamati hiyo kuwa, Wizara ya TAMISEMI inafuatilia kwa makini ujenzi wa Hospitali zote 67 za Wilaya zinajengwa kwa awamu ya kwanza kwa ukaribu na kuhakikisha zinaanza kufanya kazi, pamoja na kuhakikisha ushauri wote uliotolewa na Kamati unazingatiwa na kufanyiwa kazi. Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt Chitopela amesema, Hospitali hii ni tegemea kubwa kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa kuwa inategemea kuhudumia wakazi zaidi ya 220,000, na kupunguza adha kubwa ya wananchi wanao safiri umbali mrefu kufuata huduma ya afya.

 Kwa upande wa wananchi wa Mbulu wamemshukuru sana Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwakumbuka na kuwaondolea adha kubwa katika sekta ya afya na hakika wamepata mkombozi na kiongozi anayejali maisha yao.

No comments:

Post a Comment