DED MNASI: WALIMU FUNDISHE KWA BIDII KUOKOA KAZI ZA WALIMU WAKUU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 12 March 2020

DED MNASI: WALIMU FUNDISHE KWA BIDII KUOKOA KAZI ZA WALIMU WAKUU


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Haji Mnasi akizungumza na walimu Wilayani Ileje mkoani Songwe na wametakiwa kufuata taratibu za kazi


 NA FREDY MGUNDA,ILEJE.
 
WALIMU Wilayani Ileje mkoani Songwe wametakiwa kufuata taratibu za kazi ili kuepusha kuwatwisha mizigo Walimu wakuu na Wakuu wa Shule.

Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ndg.Haji Mnasi alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa walimu wa Shule za Msingi za Kata za Itumba na Isongole yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Nyerere mjini Itumba.

“Warahisisheni Walimu Wakuu msiwape kazi ya kushitaki kwa usumbufu na kufikia kukataliwa na baadhi ya walimu kwasababu ya usumbufu wenu”alisema kiongozi huyo.

Mnasi aliongeza kuwa,katika ziara za kikazi alizozifanya kwenye baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari aliojionea hali isiyo ya kuridhisha ambayo inaonesha uwajibikaji wa kiwango cha chini kinachoathiri hata matokea ya mitihani ya kitaifa.

Katika kikao hicho pia alipongeza idara zote zinazohusika na masuala ya elimu kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika kwenye kata zote za wilaya hiyo.

Kwa miaka ya hivi karibuni wilaya ya Ileje imekuwa ikifanya vibaya kwenye mitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi hali iliyopelekea viongozi hawa kukutana na walimu katika kukumbushana mbinu za kujifunzia na kufundishia.


No comments:

Post a Comment