BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI MADINI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 20 March 2020

BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI MADINI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

Baadhi ya wachimbaji wadogo wa Almasi katika Kata ya Magazo Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga (kulia), wakisalimiana na Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa kwanza kushoto) alipotembelea eneo la kuchenjulia mabaki ya mchanga wa almasi (makinikia) kutoka mgodi wa Mwadui/ Williamson Diamonds Ltd. Wachimbaji hao wamechukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuvaa vikinga pua na mdomo (mask).
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa mgodi wa Mwadui/ Williamson Diamonds Ltd (kushoto) alipotembelea mgodi huo kujionea zoezi la utoaji nje mabaki ya mchanga wa almasi (makinikia) kwa ajili ya kuchenjuliwa upya na wachimaji wadogo.
 Mkuu wa Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba (katikati) akionesha namna sahihi ya kutakasa mikono kwa kutumia sabuni maalum (hand sanitizer) ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wilayani Kishapu kukagua eneo la mchanga wa almasi uliotolewa na mgodi wa Mwadui (Williamson Diamonds Ltd).

 Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wilayani Kishapu akitoka kukagua eneo la mabaki ya mchanga wa almasi uliotolewa kwa wananchi na mgodi wa Mwadui (Williamson Diamonds Ltd) ili kuchenjuliwa upya.

Waziri wa Madini, Doto Biteko akikagua vizimba vilivyoandaliwa kwa ajili ya shughuli ya kuchenjua mabaki ya machanga wa almasi (makinikia) katika eneo la Maganzo wilayani Kishapu. 

Zoezi la utoaji mabaki ya mchanga wa almasi (makinikia) kwa ajili ya kuchenjuliwa upya na wananchi katika eneo la Maganzo limeanza Machi 19, 2020.

 Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wilayani Kishapu akikagua eneo ambalo wananchi watakuwa wakitakasa mikono yao kwa sabuni maalum (hand sanitizer) kabla ya kuingia eneo la kuchenjulia mabaki ya mchanga wa almasi (makinikia) ikiwa ni tahadhari dhidi ya virusi vya Corona.

 Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akikagua vifaa vya kupima ubora wa almasi katika eneo la mnada wa uuzaji madini hayo lililopo katika mgodi wa Mwadui unaomilikiwa na kampuni ya Williamson Diamonds Ltd.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Mwadui/ Williamson Diamonds Ltd, Ayound Mwenda (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu vifaa vya kupimia ubora wa alamsi mgodini hapo.


Na George Binagi-GB Pazzo, Shinyanga

WAZIRI wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wa madini nchini Tanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa mafua, kikohozi na homa kali ya Corona ambao umesababisha athari ikiwemo vifo katika mataifa mbalimbali duniani.

Biteko alitoa tahadhari hiyo Machi 19, 2020 alipotembelea eneo la kuchenjulia mabaki ya mchanga wa almasi (makinikia) uliotolewa na mgodi wa Mwadui (Williamson Diamonds Ltd) kwa wachimbaji wadogo ambapo alifurahishwa na matayarisho mazuri ya eneo hilo ikiwemo tahadhari dhdi ya virusi vya Corona kabla ya zoezi la kuchenjua mchanga huo halijaanza rasmi.

“Tuendelee kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuepuka kushikana mikono ovyo, lakini pia tuzingatie matuzi sahihi ya viziba pua na mdogo (mask) pamoja na kutakasa mikono kwa kutumia sabuni maalum (hand sanitizer)” alisisitiza Biteko wakati akisalimiana na baadhi ya wachimbaji wadogo wa almasi katika eneo la Maganzo.

Aidha Biteko aliwakumbusha wafanyabishara na wachimbaji wadogo wa almasi kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria na kanuni za madini ikiwemo kuuza madini yao kwenye masoko huku wakijiepusha na utoroshaji madini kwani yeyote atakayeshindwa kufanya hivyo ataangukia mikononi mwa sheria na kuishia kufungwa jambo ambalo asingependa litokee.

“Ni marufuku kutunza kinyemera madini nyumbani kwako bila kuwa na nyaraka kutoka kwa maafisa wetu wa madini, sisi tukikukamata hayo madini yatakuwa mali halali ya Serikali” Biteko aliwatahadharisha wafanyabishara na wachimbaji wa almasi.

Awali akizungumzia zoezi la utoaji nje mchanga wa almasi, Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa Shinyanga (SHIREMA), Greygory Kabusi alisema maandalizi yamekamilika na vikundi 700 vya wachimbaji wadogo wa almasi vyenye wanachama 10 kila kimoja vinatarajiwa kuanza shughuli ya kuchenjua mchanga huo na hivyo kujipatia kipato.

Naye Mkuu wa Wilaya Kishapu, Nyabaganga Talaba alisema Serikali inafuatilia kwa ukaribu zoezi la uchenjuaji mchanga huo ili kuchukua tahadhari za kiusalama hususani katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya Corona.
Tazama video hapa chini

No comments:

Post a Comment