ARUSHA YAOMBA KUIDHINISHIWA MAPENDEKEZO YA BAJETI YA BILION 298.0 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 24 March 2020

ARUSHA YAOMBA KUIDHINISHIWA MAPENDEKEZO YA BAJETI YA BILION 298.0

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Monduli Idd Kimanta akiongoza kikao cha sekretariet ya mkoa huo iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha picha na Ahmed Mahamoud Arusha 

Wajumbe wa sekretarieti ya mkoa wa Arusha wakifuatilia hotuba ya Kaimu Mwenyekiti wa kikao hicho Dc Idd Kimanta kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro aliyeinamisha kichwa Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo na Afisa wa uchumi Jiji la Arusha pembeni ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.



MKOA wa Arusha,umepitisha mapendekezo ya bajeti ya shilingi 298 ,016,631,500 kwa  mwaka 2020/21 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma za jamii

Akiwasilisha mapendekezo hayo kwenye kikao cha Kamati ya ushauri ya mkoa,RCC, kilichofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa, Afisa mipango wa mkoa, Melichiory Temu, amesema kati ya fedha hizo halmashauri za wilaya zitatoa shilingi 42,592,000,000.

Amesema mwaka 2019/20 mkoa huo uliidhinishiwa shilingi 263,152,019,925kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeo.Amesema mwaka huu mkoa unatarajiwa kukusanya shilingi 42 592,000,000 kutoka katika vyanzo mbalimbali .

Amesema mapato yameshuka kwenye halmashauri mbili za Arusha DC na Monduli ,kutokana na sababu mbalimbali

Amesema Halmashauri ya Arusha DC ,mapato yake yameshuka kwa asilimia 16.8 %  kutokana ikiwemo mapato ya huduma ya maji kuhamishiwa kwenye mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha AUWSA

Aidha Wilaya ya Monduli mapato yameshuka kwa asilimia 9.2% kutokana na baadhi ya kampuni zilizosajiliwa na EPZ kutakiwa kisheris kulipa ushuru kwenya Mamlaka ya mapato nchini TCRA, badala ya halmashauri ya wilaya.

Amesema sababu nyingine ya kushuka kwa mapato ya halmashauri hizo ni mabadiliko ya kisheria kuwapa wakulima wakubwa uhuru wa kuchagua kati ya kulipa Service levy kwa asilimia 0.3% au Produce cess asimia 3% Mabadiliko ya matumizi katika shamba la Burka lenye ukubwa wa ekari 75,000 ambalo kwa asa wamiliki wake wameng’oa mibuni.

Amesema kutokana na mabadiliko hayo halmashauri zinajipanga  kushughulikia upya  upungufu huo kwa kuibua vyanzo vipya vya mapato.

Akichangia kwenye kikao hicho mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Kimanta, ambae alikuwa ni mwenyekiti wa kikao hicho cha ,RCC, amewapongeza Viongozi wa vyama vya siasa mkoa wa Arusha,walioalikwa kushiriki kakao hicho,kwa michango yao na kusema kuwa huo ni ukomavu wa kisiasa. 



No comments:

Post a Comment