MAHARI: 'MUME WANGU HAWEZI KUNINUNUA' - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 2 February 2020

MAHARI: 'MUME WANGU HAWEZI KUNINUNUA'





"SICHUKULII mahari kama malipo yangu ... kwa sababu Geoffrey hawezi kunilipa," amesema Angela, raia wa Uingereza mwenye asili ya Ghana anaelezea utamaduni maarufu sana katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. 

"Badala yake napenda dhana iliyopo kwamba mchumba wangu na familia yake wananichukulia kama mtu wa thamani ninayejiunga na familia yao."

Mahari hutolewa wakati ambapo ya mume mtarajiwa anataka kuoa mahali fulani, mume mtarajiwa uagizwa na wakwe zao watarajiwa mambo gani anapaswa kuyaandaa kabla ya harusi yao.

Mahitaji ambayo ataelezwa kuleta kabla huwa ni fedha au zawadi, au vyote viwili.

Mara nyingine mahitaji hayo yanaweza kupelekwa kwa wakati mmoja lakini mara nyingi mahari hailipwi kwa pamoja.

Pia utamaduni huu ni maarufu sana Thailand, China na Papua New Guinea.

Lkini kwa upande wa Angela ni suala tu la kukubali alipotoka.

"Waafrika huona fahari sana na utamaduni wao kutoa na kupokea mahari. Kulikuwa na wakati ambao kuwa mwafrika halikuwa jambo la kuvutia. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika na wenyeji wanajivunia utamaduni wao wa Kiafrika."

Mume wake Geoffrey, ambaye pia ni Muingereza mwenye asili ya Ghana, anaelezea utamaduni wa kulipa mahari kama kutoa shukrani kwa familia ya mke.

"Lakini iwapo malipo yatakuwa ya juu sana na kuondoa ile ishara ya shukrani, kuna hatarisha mchakato mzima kwa sababu unaondoa maana ya mahari."

'Wewe hauuzwi, kwasababu hakuna anayeweza kukunua'

Wiki moja kabla ya ndoa yao, Geoffrey na Angela waliandaa sherehe ya harusi ya kitamaduni nchini Ghana.

Ni wakati wa sherehe kama hiyo ambapo mahari hulipwa - ama iwe pesa au zawadi - ilikabidhiwa kwa familia ya Angela.

Lakini wanandoa hao waliamua kubadilisha sherehe yao na kuifanya kuwa ya kisasa zaidi: "Ile mahari itakayotolewa baadaye tutapewa sisi wanandoa.

"Mama yangu amekuwa muwazi na kuanzia mwanzo alikuwa akisema 'Wewe siyo wa kuuzwa, hakuna anayeweza kukunua'."

Gharama ya mahari inatofautiana Geoffrey anasema: "haikuwa ghali hivyo - ilikuwa katika kundi la mamia."
Lakini kwa wanandoa wengine Blessing na Chelsea, waliamua kuangazia mahari yao kwa mtazamo tofauti.

Blessing (kushoto) anasema alilazimika kufanya kazi siku saba kwa wiki ili kuweza kulipa mahari

Blessing, mwenye asili ya Zimbabwe, anasema alilazimika kutafuta kazi ya pili ili aweze kulipa mahari aliyoitishwa: "Nitasema tu kwa ujumla, ni kiasi ambacho naweza kuanza malipo ya pole pole ya kununua nyumba Uingereza."

Awali, Chelsea alikuwa ameondoa uwezekano wa kufanya harusi ya kitamaduni kwasababu baba yake aliaga dunia.

"Nilijiuliza… ni nani atakayechukua pesa zangu? kwasababu hizo huchukuliwa na baba na mama.
Lakini Blessing akafalu kumshawishi mkewe aendelee na maandalizi ya harusi yao ya kitamaduni licha ya kiasi kikubwa cha pesa ambacho aliombwa kulipa, aliamini kwamba mahari ni kitu cha msingi.

Anasema iwapo angeshindwa kulipa mahari aliyoitishwa, hangeweza kukutana na familia ya mke.
Haifahamiki ni lini mahari ilikuwa jambo la lazima Barani Afrika lakini nchi nyingi siku hizi hupendelea pesa.

Kihistoria, ulipaji wa mahari unatofautiana kulingana na nchi na utamaduni wa eneo.

Evelyn Schiller anaona siku hizi watu wengi wanachukulia mahari kwa mfumo wa pesa zaidi kuliko zawadi

Mwanaharakati Evelyn Schiller anapinga utoaji wa mahari Uganda. Anaamini kwamba kigezo cha mahari kimebadilika katika kipindi cha vizazi vitatu vilivyopita.

"Tazama kwa wakati huu, mahari ilivyo. Inachukuliwa kwa misingi ya pesa na hapo ndipo neno malipo linapotokea. Siyo tena zawadi kwa bibi harusi badala yake imekuwa kama malipo kwa bibi harusi."

2015, mahakama ya juu zaidi ya Uganda ilitoa uamuzi kwamba mahari isiwe kitu cha lazima lakini iwapo wanandoa watakuja kutalakiana, mtu kudai arejeshewe mahari aliyotoa ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo utoaji wa mahari umekuwa ukiendelezwa kwasababu kunachukuliwa kama njia moja ya kuimarisha uhusiano baina ya jamii.

Mtangazaji wa BBC Tolly T anaamini kwamba mahari ni sawa na umiliki


Watu weusi Uingereza tuna utamaduni wetu kwa sasa'

Mtangazaji raia wa Uingereza mwenye asili ya Nigeria,Tolly T, amekuwa akihoji ikiwa utamaduni wa utoaji mahari unaweza kuzaa matunda kwake: "Hasa… ni kutoa pesa kwa watoto wangu. Unahisi kuwa mmiliki."

Lakini je mahari ina uhusiano wowote na kuwa mke mwema kwa Tolly T?

"Kwa waliozaliwa miaka ya 80 kuendelea kama sisi, Waingereza weusi, au wenye asili ya Nigeria ama hata bila kujali chimbuko lako, tumekuwa na utamaduni wetu," amesema.

"Tunaendeleza kile tunachotaka kutoka Afrika na kufanya vivyo hivyo kutoka Uingereza. Kisha tunajiundia utamaduni wetu ambao unaturuhusu kujiuliza maswali na kuutekeleza kama ni wenye kuwa msingi kwetu sisi."

-BBC

No comments:

Post a Comment