MAMLAKA
ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) imetoa cheti kwa Ofisi ya
Binafsi ya Waziri Mkuu baada ya kufanyia ukaguzi katika maeneo yote ya
ofisi hiyo na kuonesha kuwa yamekidhi viwango.
Cheti
hicho kimetolewa jana jioni (Jumamosi, Februari 1, 2020) na Kaimu
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda na kupokelewa na Katibu wa
Waziri Mkuu Bw. Raymond Gowelle.
Akikabidhi
cheti hicho, Bi Khadija aliipongeza Ofisi hiyo kwa kuonesha mfano wa
uetekelezaji wa sheria, ambapo amezishauri ofisi nyingine za umma ziige.
“Ofisi
Binafsi ya Waziri Mkuu imeonesha mfano wa kuigwa kwa utekelezaji wa
sheria, kwani walituita tukaja kufanya ukaguzi na tukatoa maelekezo ya
namna ya kuboresha baadhi ya maeneo na wamerekebisha.”
Alisema
baada ya kutekeleza maelekezo hayo suala lililokuwa limebakia ni
upimaji wa afya kwa wafanyakazi pamoja na kutoa mafunzo ya huduma ya
kwanza ambayo yamefanyika leo (jana).
Mtendaji
huo alisema ni muhimu kwa ofisi zote kuzingatia sheria ya Usalama na
Afya Mahali pa Kazi kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria.
Baada
ya kukamilisha zoezi la upimaji wa afya na mafunzo ya OSHA, pia
watumishi wa Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu walikumbushwa namna bora ya
kufanyakazi kwa uadilifu. Mafunzo yalitolewa na watalaamu kutoka Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, FEBRUARI 2, 2020.
No comments:
Post a Comment