"Sababu kubwa ya tangazo hilo si kwa sababu ya kile
ambacho kinatokea China kwa sasa lakini kile ambacho kinatokea katika mataifa
mengine," alisema kiongozi mkuu wa shirika la afya duniani Tedros Adhanom
Ghebreyesus .
Kinachoangaziwa zaidi ni kuhusu ugonjwa huo kusambaa mataifa
mengine huku kukiwa na mfumo duni wa afya
Watu takribani 213 wamefariki kutokana na virusi hivyo
nchini China.
Shirika la afya duniani limesema kuwa kumekuwa na visa 98
katika mataifa mengine 18 ingawa hakuna vifo vilivyobainika. Visa vingi vya
wagonjwa hao walikuwa wamesafiri kutoka mji wa Wuhan, eneo ambalo mlipuko wa
ugonjwa huo ulianza.
Hata hivyo kuna kesi nane zilizosababishwa na maambukizi ya
kati ya mtu kwa mtu huko Ujerumani, Japan, Vietnam na Marekani.
Akizungumza katika mkutano wa habari Geneva, Dkt Tedros
alielezea virusi vya corona kuwa mlipuko wa ugonjwa ambao haujawahi kutokea
awali na bado haujaweza kupata suluhu.
Dkt.Tedros alisifia hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na
serikali ya China katika kuzuia maambukizi yasienee na alisema kuwa hakukuwa na
sababu ya kuzuia watu wasisafiri au biashara zisiendelee.
"Lakini nataka kueleweka kuwa ,tangazo hili
halimaanishi kuwa ni kura ya kutoiamini China".
Lakini nchi mbalimbali zimechukua hatua ya kufunga mipaka na
kusitisha safari za ndege za nchini China, vivyo hivyo makampuni makubwa pia
yamefunga maduka yao.
Itakuwaje kama virusi hivi vitasambaa katika mataifa
mengine? Mataifa ambayo uchumi wake uko chini au wa katikati na ngumu kwa wao
kupata vifaa vya kujizuia maambukizi au kutafuta tiba.
Hofu ipo kuwa inawezekana ugonjwa huu ushindikane kuzuilika
na unaweza kumpata mtu bila kujijua wakati mwingine.
Kumbuka kuwa ugonjwa huu umeanza mwezi mmoja tu mpaka sasa
na tayari kuna kesi 7,736 zimethibitishwa kuwepo nchini China na watu wakiwa
wanashukiwa kuwa na ugonjwa huo.
Mwaka 2014, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ulitokea magharibi
ya Afrika, ugonjwa huo uliweka historia kubwa katika maisha ya binadamu, na
ulionyesha wazi ni namna gani nchi maskini zinavyoweza kushambuliwa na mlipuko
wa ugonjwa.
Na kama hali kama hii ya virusi vya ebola ingetokea katika
maeneo ya aina hiyo ingekuwa ngumu sana kuzuia maambukizi.
Tuko kwenye hatua ambayo asilimia 99 ya kesi za watu wenye
maambukizi iko China na shirika la afya duniani lina imani kuwa nchi hiyo
inaweza kukabliana na mlipuko huo.
Lakini kutangaza kuwa janga la dharura la dunia kutaweza
kuruhusu WHO kuzisaidia nchi zenye kipato kidogo na cha katikati kujiandaa
kukabiliana na virusi vya corona.
-BBC
No comments:
Post a Comment