NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA KWENYE BLACK HISTORY MONTH, UJERUMANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 31 January 2020

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA KWENYE BLACK HISTORY MONTH, UJERUMANI

Black History Month Hamburg Germany.

The Ngoma Africa Band on action 2019.

BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya "The Ngoma Africa Band" aka FFU-Ughaibuni alimaarufu pia kwa majina ya utani kama viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" inayoongozwa na mwanamuziki Ras Makunja ya nchini Ujerumani, inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho kubwa la kufungua mwezi.

Akitoa taarifa hizo kiongozi wa bendi hiyo alisema onesho hilo litafanyika katika tamasha la 'Black History Month' litakalofanyika jijini Hamburg Februari Mosi, 2020 katika ukumbi wa Grunspan.

Ngoma Africa Band imeweka rekodi ya kuwa bendi ya muziki ya kigeni inayodumu kwa miaka 27 barani ulaya na katika mmajukwaa ya kimataifa ,ilianzishwa mwaka 1993 ka kiongozi wake kamanda Ras Makunja. Kufuatilia zaidi tembelea https://www.youtube.com/watch?v=oTD5ckMYUtM

No comments:

Post a Comment