SERIKALI KUENDELEA KUTAIFISHA MALI ZA WALA RUSHWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 31 January 2020

SERIKALI KUENDELEA KUTAIFISHA MALI ZA WALA RUSHWA

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas.

MSIMAMO wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mageuzi ya kimfumo na kitaasisi, umesababisha Tanzania kuwa miongoni mwa vinara katika vita dhidi ya rushwa duniani.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema hayo akirejea utafiti uliyofanywa na Transparency International mwaka jana na kutangazwa Januari 23 Mwaka huu.

Amesema Tanzania imekuwa ya 96 duniani tofauti na Mwaka 2017 ilipokuwa ya 103 na ya 117 Mwaka 2015. Kwa Afrika Mashariki Tanzana inatajwa na ripoti ya sasa kwamba ni ya Pili kwa kutokuwa na vitendo vya rushwa, ikitanguliwa na Rwanda.

Ametaka ikumbukwe katika kipengele cha juhudi za kupambana na rushwa, Julai mwaka jana Tanzania ilikuwa ya Kwanza kati ya Nchi 15 za Afrika, ambazo zilizofanyiwa utafiti na taasisi za Transparency na Afrobaramoter.

“Siyo siri kwamba haya ni mafanikio makubwa yanayotokana na msimamo wa Rais, Dkt. Magufuli katika vita hii ikiwemo kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na kuchukua hatua haraka hasa yanapotendeka makosa ya uhujumu uchumi,” amesema Dkt. Abbas.

Amesema Serikali katika vita dhidi ya vitendo vya rushwa, imefikia hatua ya kutaifisha mali zote zinazothibitika kwa mujibu wa sheria kwamba zimetokana na rushwa.

Kwa mujibu wake, mali mbalimbali zikiwemo nyumba, magari na fedha taslim za waliothibitika mahakamani kuwa zilitokana na rushwa zimerudishwa serikali na kwamba hata msimamo wa Rais, Dkt. Magufuli hautabadilika katika suala hilo.

No comments:

Post a Comment