MADAKTARI BINGWA WA CUBA, KUIMARISHA HUDUMA BENJAMIN MKAPA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 31 January 2020

MADAKTARI BINGWA WA CUBA, KUIMARISHA HUDUMA BENJAMIN MKAPA

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).

HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH) Leo imesaini mkataba wa ushirikiano na Nchi ya Cuba, ambao utawezesha wataalamu bingwa wa afya kuja nchini. Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dk. Alphonce Chandika amesema makubaliano hayo yanasema wataalam wasiopungua Saba, wanatarajiwa kuja katika awamu ya kwanza.

Ametaja maeneo yaliyopewa kipaumbele na mpango huo wa kuongezea nguvu wataala waliopo hospitalini, kuwa ni Upasuaji ambako watapokea Daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo pamoja na bingwa wa dawa za usingizi.

Kitengo cha Maabara ya Moyo, watapelekewa Daktari bingwa, Kitengo cha Uchunguzi wa Mfumo wa Chakula, watapokea Daktari bingwa na Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) wapelekewa Daktari bingwa na Muuguzi.

Wataalamu wote ni wa daraja la kwanza, wenye viwango vya kimataifa na amesema watawasili ndani ya muda usiyozidi miezi miwili kuanzia sasa.

Amesema makubaliano hayo ni mwanzo wa hatua ya BMH kufanyia usaili wataalam hao, ili kujiridhisha na sifa zao.

Baada ya awamu ya kwanza, amesema makubaliano hayo yanasema BMH wataweza kupeleka maombi na kupatiwa wataalamu wengine kila watakapowahitaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dkt. Chandika, akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari, muda mfupi kabla ya kusaini mkataba wa ushirikiano na Cuba, jijini Dodoma Leo.
Dkt. Chandika amesema gharama za kupata mtaalamu mwenye viwango vya mabingwa hao ni kubwa, BMH hawawezi kumudu lakini imewezekana kutokana na urafiki wa kiwango cha udugu, uliopo baina ya Tanzania na Cuba.

Amesema chimbuko la uhusiano huo ni urafiki wa kiwango cha udugu uliyokuwepo kati waasisi wa mataifa hayo; hayati Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na hayati Fidel Castro.

“Yaani gharama zinazotumiwa kwa mtaalam Mmoja na nchi nyingine zenye wataalam wa aina hii, kwetu zitatumiwa kwa wataalam Wanne; sana tutagharamia kuwawezesha kuishi na kufanya kazi nchini,” amesema.

Naye Balozi wa Cuba nchini, Lucas Domingo amesema anafurahi kuona uhudiano wa kihistoria kati ya nchi hizo, unaendelea kuimarika kupitia sekta mbalimbali, ikiwemo ya afya.

Makubaliano hayo yametiwa saini na Dkt. Chandika pamoja na Kiongozi wa Timu ya Madaktari kutoka Cuba, Dkt. Juan Miguel, wakishuhudiwa na Balozi, Prof. Domingo na Afisa mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Dkt. James Charles.

No comments:

Post a Comment