Na Anitha Jonas – WHUSM
WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amewataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kuwa wawazi katika mijadala ya mkutano huo kwa mambo ambayo hayaendi vizuri.
Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wenye lengo la kukumbushana, kuelimishana na kuweka mazingira bora ya utendaji kazi na kuweka umoja kati ya wafanyakazi na viongozi wa menejimenti.
“Katika Baraza hili ningependa muwe wawazi katika mijadala ya mambo yote yanayokwamisha utendaji wa majukumu ya wizara lengo ni kuhakikisha mazingira ya utendaji yanaboreshwa na kazi zinafanyika kwa manufaa ya taifa kwa wizara hii inamambo mengi yanagusa jamii moja kwa moja na hasa vijana tukiangalia sekta ya mfano Sanaa na Michezo,”alisema Dkt.Mwakyembe.
Naye Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi aliwasitiza wafanyakazi wa waadilifu, kuepuka ubadhirifu na kufuata kanuni na taratibu za utumishi wa umma kwa kufanya hayo itasaidia kujenga mazingira yenye manufaa kwa wananchi na taifa kwa jumla.
“Mkutano wa baraza ni muhimu kwani unawaleta wafanyakazi na menejimenti pamoja hivyo basi kikao hichi kisitumimike kutafuta umaarufu badala yake utumike kujadili kwa kina namna ya kuboresha mazingira ya utendaji na mikakati ya itakayosaidia kuendeleza mbele sekta za wizara,’’alisema Dkt.Possi.
Pamoja na hayo Dkt.Possi liwasisitiza wajumbe hao wa baraza kutoa hoja zenye tija na maslahi kwa wizara huku akisema nimatarajio yake kuwa kikao hicho kitaibua fursa za namna ya kuboresha wizara na utendaji.
Halikadhalika nae Mwenyekiti wa Tughe Tawi la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Mfaume Saidi aliushukuru uongozi wa wizara kwa kuboresha utendaji na kuimarisha kuimarisha ushirikiano kwa wafanyakazi.
No comments:
Post a Comment