TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 31.01.2020: WANYAMA, GIROUD, MERTENS, MATIC, CAVANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 31 January 2020

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 31.01.2020: WANYAMA, GIROUD, MERTENS, MATIC, CAVANI

Celtic wameonesha nia ya kutaka kumsajili Wanyama

Tottenham wapo tayari kumuuza kiungo mkabaji raia wa Kenya Victor Wanyama, 28, kwa klabu yoyote itakayofikia dau la pauni milioni 8. Klabu ya Celtic imeonesha kuvutiwa kumsajili kiungo wake huyo wa zamani. (Mirror).

Klabu ya Lazio ya Italia inataka kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa na klabu ya Chelsea Olivier Giroud, 33. (Sky Sports).

Chelsea pia wanatarajiwa kupeleka ofa ya pili ya usajili kwa mshambuliaji wa Napoli na Ubelgiji Dries Mertens, 32, baada ya ofa ya kwanza kukataliwa. (Telegraph)


Nemanja Matic amekuwa mhimili wa kutegemewa kwenye safu ya kiungo ya Man United.

Kiungo mkabaji wa Serbia Nemanja Matic, 31, amegoma kuihama klabu ya Manchester United na yupo tayari kusaini mkataba mwengine wa kumbakisha Old Trafford. (Telegraph).

Manchester United wamepewa nafasi ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Brazil Willian Jose, 28, kutoka klabu ya Real Sociedad. (Sky Sports).

United pia imefeli kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Joshua King, 28. (Telegraph)

Kumekuwa na mvutano wa bei ya mauzo ya Cavani baina ya PSG na Atletico

Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32, hataihama klabu ya Paris St-Germain katika dirisha la usajili linalofungwa leo. (L'Equipe - in French).

Mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller anaweza kuihama klabu yake ya Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 30 amekuwa na klabu hiyo kwa kipindi chake chote cha uchezaji lakini kwa sasa hana raha kwa kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza. (Bild - in German)

Cedric Soares

Arsenal wanapanga kukamilisha usajili wa mkopo wa beki wa kulia wa Southampton na Ureno Cedric Soares, 28. (Standard)

Southampton hawataki kumuuza kiungo na kapteni wao raia wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 24, japo klabu ya Tottenham imeonesha nia ya kumtaka. (Star)
 

-BBC

No comments:

Post a Comment