PAROKO ASISITIZA UPENDO, UMOJA NA USHIRIKIANO KWA JAMII - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 26 January 2020

PAROKO ASISITIZA UPENDO, UMOJA NA USHIRIKIANO KWA JAMII

Mbunge wa Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa akifafanua jambo kwenye ibada ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mapadre wa Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo mitume Nyamilangano Ushetu.

Sehemu ya waumini wakifuatilia ibada ya harambee ya ujenzi wa nyumba ya mapadre katika Parokia ya Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo mitume Nyamilangano Ushetu.

Baadhi ya waumini wakifuatilia ibada ya harambee ya ujenzi wa nyumba ya mapadre katika Parokia ya Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo mitume Nyamilangano Ushetu.

Mbunge wa Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa akizungumza kwenye ibada ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mapadre wa Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo mitume Nyamilangano Ushetu.

Harambee hiyo pia imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw. Anamringi Macha pamoja na wageni mbalimbali.

PAROKO wa Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo mitume ya Nyamilangano Ushetu wilayani Kahama, Severine Mshumbuzi amezungumzi umuhimu wa jamii kuishi kwa upendo, umoja na ushirikiano ili kufikia maendeleo ya kweli.

Akizungumza kwenye ibada ya harambee ya kujenga nyumba za mapadre wa  parokia hiyo amesema jamii zikiishi kwa upendo, haki na  umoja mafanikio ya kanisa na jamii yatafikiwa haraka. Katika harambee hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Ushetu na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa zaidi ya shilingi milioni 22 zilipatikana.

Naye Mbunge wa Njombe Mhe. Hanz Mwalongo amewataka Wakristo katika Jimbo la  Ushetu kufanya kazi kwa bidii na kumtolea Mungu sadaka kamili ili kujiwekea hazina ya kutosha Mbinguni.

Kwa upande wake, Mbunge wa Ushetu na Naibu Waziri wa Ujenzi amewataka wakazi wa Ushetu kuwa wacha Mungu na wakarimu ili kuvutia wageni na wawekezaji wengi kuwekeza katika jimbo hilo.

Harambee hiyo pia imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw. Anamringi Macha pamoja na wageni mbalimbali.

No comments:

Post a Comment