MAWAKALA ACT-WAZALENDO ZANZIBAR WAMGEUKA MAALIM SEIF - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 20 January 2020

MAWAKALA ACT-WAZALENDO ZANZIBAR WAMGEUKA MAALIM SEIF

Maalim Seif Shariff Hamad.

Na Mwandishi Wetu, Pemba
MAWAKALA wa Chama cha ACT –Wazalendo, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar wameipongeza Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kwa kutekeleza majukumu yao kwa uwazi, uadilifu na umakini kazi ya uandikishaji wapigakura katika Daftari la kudumu la wapigakura.
Wakizungumza kwenye vituo vya uandikishaji wapigakura kwa nyakati tofauti wilayani Micheweni, Mawakala hao walisema wanaridhishwa na kazi hiyo. Hamad Rashid Hamad ambaye ni wakala wa chama hicho kwenye Kituo cha Wingwi Njuguni, alisema uandikishaji huo unakwenda vizuri, wanapata ushirikiano mkubwa kutoka ZEC.
“Kituo kimefunguliwa mapema, saa 2:00 tumeanza kazi, hadi sasa hakuna matatizo mambo yanakwenda kama yalivyopangwa kama unavyoona mwenyewe,” alisema Hamad.
Katika Kituo cha Konde, wakala mwingine wa chama hicho, Khamis Ali Khalid, alisema ZEC imejipanga vizuri kuanzia vifaa vya uandikishaji, utaratibu wa uandikishaji na ushirikiano kwa mawakala. 
Khamis Omar Idd wa Kituo cha Tumbe Magharibi, alisema uandikishaji unakwenda vizuri, wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kujiandikisha katika kituo hicho.
Katika Kituo cha Micheweni, Elias Ameir aliipongeza ZEC kwa maandalizi mazuri, vifaa vya uhakika vya uandikishaji pamoja na kufunguliwa kwa wakati kituo hicho.
Hali kama hiyo pia imeelezwa na Wakala wa ACT-Wazalendo katika Kituo cha Shumba Vyamboni, Khamis Mohammed Khamis akielezea kuridhishwa kwake na kazi ya uandikishaji wapigakura katika daftari la kudumu.
Maelezo ya Mawakala hao yanaonekana kutofautiana na tuhuma zilizotolewa na viongozi wa ACT-Wazalendo Kisiwani Pemba.
Mshauri Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad alidai kuna watu wengi wasiokuwa na vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi na kudai wanaweza kukosa haki ya kujiandikisha jambo ambalo Mawakala wa chama chake wanalielezea tofauti.

Wilaya ya Micheweni kuna vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi vimetekelezwa katika Ofisi za Wilaya za Wakala wa Usajili Matukio ya Kijamii Zanzibar licha ya kutolewa kwa matangazo mara kadhaa kuwataka wahusika wajitokeza kuvichukua lakini hakuna aliyekwenda. 

No comments:

Post a Comment