Msanii Florence Shirima anayefanya spoken words kwenye jukwaa la KAN. |
Msanii Saitoti Alakaila wa Warrios from The East akitumbuiza kwenye tamasha la KAN. |
Msanii Lwanda Ataka wa Warriors from The East akitumbuiza wkati wa tamasha. |
Msanii Amina kutoka Siti & The Band akitumbuiza kwenye jukwaa la KAN. |
Add caption |
Msanii Sandra Nankoma kutoka Uganda akitumbuiza. |
UBUNIFU uliotumika kutengeneza jukwaa kuu la Knowledge, Art na
Networking (KAN) umekua kivutio kikubwa kwa wapenzi wa sanaa na burudani ya
kupambwa na miamvuli ya rangi tofauti tofauti ikisindindikizwa na michoro
inayong'ara ikionesha watu wakicheza kwenye ukuta wa jukwaa.
Akizungumza kuhusu jukwaa hilo Mkurugenzi wa tamasha hilo Dave
Ojay amesema kupamba jukwaa hilo na baadhi ya maeneo mengine kwa kutumia
miamvuli kunaendana na kauli mbiu ya mwaka huu Maendeleo ni watu si vitu.
Alisema, miamvuli imechukuliwa kama mfano wa mti unaoleta kivuli
kwenye maisha ya watu. Sanaa inayotumika kuchora maua yanayopambwa na rangi
tofauti tofauti kwenye mwamvuli inawakilisha 'art' pamoja na vyuma vinavyofunguka na kufunga mwamvuli
ukifunguka unawakilisha 'network' .
"Ubunifu wa kupamba kwa kutumia miamvuli inaendana na kauli
mbiu ya tamasha ambapo sanaa ya kupata maua kwwenye miamvuli hiyo pamoja na
vyuma vinavyoachana na kushikana wakati mwamvuli ukifungwa na kufunguliwa
viinashiria nertworking," alisema Ojay.
Kivuli cha miamvuli kinatasfiri maendeleo ya maisha ya mtu kama
ilivyo kauli mbiu inayojadili mambo mbalimbali ya maendeleo yanahitaji pia
kivuli ikiwa ni pamoja na malazi, makazi na chakula.
Msimu wa pili wa tamsha hili ulianza tatehe 22 na unafika kileleni
leo ambapo wasanii wanne watahitimisha kufungwa kwa tamasha hilo. Wasanii hao
ni Fid Q, ktuoka Tanzania, Isabella Novella kutoka Mozambique, Victor Kunonga
kutoka Zimbabwe, Bengatronics an Tear Drops kutoka Kenya.
No comments:
Post a Comment