Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo akizungumza na Mtaalamu wa Maabara Bi. Happyness Nyaruke wakati alipotembelea kituo cha Afya Sokoine Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo, akikagua Kituo cha Afya Sokoine Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi (wa nne kulia) akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo, akipata maelezo ya ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.
Mkutano ukiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Edward Mpogolo akizungumza na watumishi waliohudhuria kwa ajili ya kumsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo wakati wa ziara yake katika halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo juu ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo wakati alipotembelea ofisini hapo.
Muonekano wa majengo ya halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mhe. Juma Ali Mwangi akizungumza.
Picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu, Singida
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jafo amempongeza hadharani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya eneo hilo kwa gharama ndogo sana ikilinganishwa na uhalisia.
Mkurugenzi huyo kwa kushirikiana na viongozi wenzake kupitia mfumo wa ‘force account’, wameweza kutumia kiasi cha sh. 420 milioni pekee kujenga ukumbi wa mikutano wa kisasa na wenye viwango, na 200 kujenga jengo kubwa la ofisi, huku akisisitiza kwa kuzitaka halmashauri ambazo bado hazijaanza ujenzi wa majengo ya ofisi na kumbi za kisasa za mikutano kuja kujifunza Ikungi.
Waziri Jafo akiwa kwenye ziara ya kawaida mkoani Singida, na kupata fursa ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya, na miradi mingine ya halamshauri akitokea Jijini Mwanza, alisema katika uongozi wake amepita kwenye halmashauri nyingi lakini hajawahi kukutana na jengo la ukumbi mzuri na wa kisasa kama huo wa halmahauri ya Ikungi.
“Mkurugenzi kilichonifurahisha ni namna mlivyozingatia thamani ya pesa (value for money) na ubora, nilisema nataka ofisi ya TAMISEMI ifanye mabadiliko na mapinduzi ya kiutendaji, tulikotoka huko nyuma hatukuwa na sifa nzuri, lakini leo hii kila mahali ukitazama ikiwemo hapa Ikungi huwezi kuamini,” alisema.
Alizitaka halmashauri za Kondoa na Iramba kwa kuanzia kuja kujifunza kupitia wenzao hao wa Ikungi, ambao idadi ya majengo yao yote yamegharimu sh 1.5 bilioni pekee “nataka wengine wakitaka kujenga ofisi waje kujifunza hapa, iwe duplicate kwa wengine kuja kucopy na kupaste,” alisema Jafo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Mpogolo alisema kiasi hicho cha pesa sh 1.5 bilioni kilitolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa halmashauri hiyo kwenye eneo la utawala bora.
Alisema kati ya pesa hizo sh 1.3 milioni zimetumika kujenga ofisi, nyumba ya DC, na Hospitali ya wilaya, huku Serikali ikiwa tayari imewatengea fedha nyingine zaidi ya sh. milioni 500 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa vituo vya afya vya Sepuka, Ihanja na Iyumbu.
Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi, Justice Kijazi, alisema tangu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo mwaka 2013, watumishi wa eneo hilo wamekuwa wakipanga na kukodi majengo ya watu binafsi kwa mikutano mbalimbali, ikiwemo kutumia hadi nyumba za wageni kwa shughuli za ofisi.
….alisisitiza kuwa jengo la ukumbi huo mpya na wa kisasa mbali ya kutumika kwa shughuli mbalimbali za mikutano ya kikazi, lakini pia litatumika kama kitega uchumi cha kuingizia halmashauri hiyo mapato, huku Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Juma Ali Mwangi, akimuomba Waziri Jaffo kusaidia mchakato wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya kwa ustawi wa afya ya wakazi wa eneo hilo.
Hata hivyo, pamoja na kufurahishwa na Ikungi lakini hakufurahishwa na utendaji na usimamizi wa miradi ya vituo 2 vya afya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Iramba, ambavyo kwa mda mrefu ujenzi wake umekuwa ni wa kusuasua.
“RAS (Katibu Tawala wa mkoa) mwambie RC (Mkuu wa Mkoa) nimesikitishwa sana na watu wa Iramba, pale kuna uzembe wa hali ya juu unaofanywa na DC na DED, haiwezekani fedha zimekwenda lakini bado matatizo ya kutokamilika kwa vituo hivyo viwili vya ‘ndago’ na kinampanda yakiendelea,” alisema Jafo
na kuongeza; “Natoa siku 4 leo jumanne (jana) nataka ninapoondoka hapa kufikia ijumaa nipate maelezo ya DC na Mkurugenzi wake kwanini wasiwajibishwe,” alisema.
No comments:
Post a Comment