HALMASHAURI KUU CCM YAWAPELEKA KINANA, MAKAMBA NA MEMBE KAMATI YA MAADILI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 13 December 2019

HALMASHAURI KUU CCM YAWAPELEKA KINANA, MAKAMBA NA MEMBE KAMATI YA MAADILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea katika hafla ya ufunguzi wa Kikao cha  Majadiliano cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) chenye lengo la kupokea utekelezaji wa Serikali Ilani ya uchaguzi mkuu ya 2015 na  kuandaa Ilani ya Chama hicho 2020 -2025 kilichofanyika Jijini Mwanza. Disemba 12,2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt. John Pombe akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais Dkt. Ally mohamed Sheini wakiimba wimbo wa chama na wajumbe wengine katika hafla ya ufunguzi wa Kikao cha Majadiliano cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) chenye lengo la kupokea utekelezaji wa Serikali Ilani ya uchaguzi mkuu ya 2015 na  kuandaa Ilani ya Chama hicho 2020 -2025 kilichofanyika Jijini Mwanza. Disemba 12,2019. 

Wajumbe wa Halmshauri kuu ya CCM Taifa (NEC) wakimshangili Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea katika hafla ya ufunguzi wa Kikao cha Majadiliano cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) chenye lengo la kupokea utekelezaji wa Serikali Ilani ya uchaguzi mkuu ya 2015 na  kuandaa Ilani ya Chama hicho 2020 -2025 kilichofanyika Jijini Mwanza. Disemba 12,2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) mara baada ya Kikao cha  ufunguzi wa Majadiliano chenye lengo la kupokea utekelezaji wa Serikali Ilani ya uchaguzi mkuu ya 2015 na  kuandaa Ilani ya Chama hicho 2020 -2025 kilichofanyika Jijini Mwanza. Disemba 12,2019.


HALMASHAURI Kuu ya Taifa (HKT) imeazimia kwa kauli moja na kuelekeza kwamba wanachama wao,  Abdulrahman Kinana, Mzee Yusuf Makamba pamoja na Benard Membe kwenye Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ili wajibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi.

Pia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) kimepokea, kujadili na kuridhia kwa kauli moja Taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili juu ya uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM wa kuwasamehe wanachama walioomba radhi kwake baada ya kukiri mbele yake kufanya makosa ya kimaadili yaliyokidhalilisha chama na viongozi wake mbele ya umma.

Wanachama waliosamehewa ni pamoja na ;- Ndg. Januari Makamba (Mb),    Ndg. Nape Nnauye (Mb) na, Ndg. William Ngeleja (Mb). 

Wakati huo huo, Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeazimia kwa kauli moja na kuelekeza kwamba wanachama wafuatao;-

1.    Abdulrahman Kinana
2.    Mzee Yusuf Makamba na,
3.    Benard Membe

Waitwe na Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ili wajibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi.

Awali Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (HKT) imefanya uteuzi wa majina ya Wagombea wa nafasi za Uongozi katika Chama na Jumuia kama ifuatavyo;-

1.    Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha

a.    Ndg. Batilda Salha Buriani
b.    Ndg. Zelothe Stephen Zelothe
c.    Ndg. Bakari Rahibu Msangi

2.    Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa

a.    Mafanikio Paulo Kinemelo
b.    Hilary Adelitius Kipingi
c.    Lucas Felix Lwimbo

3.    Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Mtwara

a.    Petro Mwendo Mwendo
b.    Mustafa Nguyahamba Mohamed
c.    Selemani Manufred Sankwa

4.    Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Dodoma

a.    Ndg. Damas Mukassa Kasheegu
b.    Baraka Andrea Mkunda
c.    Christopher Thomas Mullemwah

5.    Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani

a.    Mary Daniel Joseph
b.    Fredrick Gasper Makachila
c.    Samaha Seif Said

Licha ya hamasa kubwa waliyokuwa nayo wajumbe wa HKT kutokana na kazi nzuri ya Serikali ya CCM, Ndg. Magufuli amesisitiza kazi ya Urais ni ngumu sana na yeye ataheshimu utamaduni na desturi za CCM, Kanuni, Katiba ya CCM na Katiba ya Nchi na kwamba CCM ni kiwanda cha kuzalisha viongozi na kwa utaratibu ambao chama kimejiwekea kitampata mtu bora zaidi atakayepokea uongozi baada yake.

Nawashukuru sana viongozi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ya Chama chetu kwa kuzisimamia vizuri Serikali zetu mbili na hivyo kuwezesha kupatikana mafanikio makubwa katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM. Tukaendelee kujenga umoja, kuimarisha ujenzi wa Chama chetu na tunapoelekea katika chaguzi zinazokuja tukaepuke makundi, na tuendelee kuisimamia Serikali ikiwamo kukagua miradi ya kimaendeleo katika maeneo yetu, amesema Ndg. Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na, 
HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI

CHAMA CHA MAPINDUZI

No comments:

Post a Comment