WANAFUNZI WAFAIDIKA NA ELIMU YA KUWEKA AKIBA KUPITIA BENKI YA NMB - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 16 November 2019

WANAFUNZI WAFAIDIKA NA ELIMU YA KUWEKA AKIBA KUPITIA BENKI YA NMB

 Kaimu Mkurugenzi wa NMB – Ruth Zaipuna akikata keki pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya Wasichana ya Barbro Johansson Model iliyopo jijini Dar es Salaam.

KATIKA
kutambua umuhimu wa vijana ambao ni Taifa la kesho, Wanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya Wasichana ya Barbro Johansson Model iliyopo jijini Dar es Salaam, wamepata elimu ya fedha na umuhimu wa matumizi makini ya fedha ikiwemo kuweka akiba benki, walipotembelea Makao Makuu ya benki hiyo kujionea shughuli mbalimbali za kibenki kwa vitendo.

Wanafunzi wakipata elimu kutoka kwa Ofisa wa benki ya NMB- Monica Job. 

Kaimu Mkurugenzi wa NMB – Ruth Zaipuna akilishwa keki na Wanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya Wasichana ya Barbro Johansson Model iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi hao walipata nafasi ya kujifunza na kutembelea idara na vitengo tofauti ili kufahamu shughuli zao lakini pia walitembelea Tawi la NMB Ohio.
                                
Pamoja na hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna amewaasa wanafunzi hao kuwekeza nguvu zaidi katika elimu, kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatimiza malengo yao. 

Image Image
Wanafunzi wakifurahi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa NMB- Ruth Zaipuna na Mwalimu wao- Jennifer Dominick.


 Baada ya mafunzo hayo, wanafunzi wote walipata nafasi ya kufungua akaunti zitakazowawezesha kutunza fedha na kujijengea tabia ya kuweka akiba na kunufaika na huduma na bidhaa za benki ya NMB hususan Chipukizi na Mwanachuo Akaunti.


No comments:

Post a Comment