RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 03 Novemba, 2019 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imewataja walioteuliwa kama ifuatavyo; Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Charles Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG).
Bw. Kichere anachukuwa nafasi ya Prof. Mussa Juma Assad ambaye kipindi chake cha miaka 5 katika nafasi hiyo kinakwisha kesho tarehe 04 Novemba, 2019. Kabla ya Uteuzi huo Bw. Kichere alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Katarina Tengia Revocati kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.
Kabla ya uteuzi huo Bi. Katarina Tengia Revocati alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na anachukua nafasi ya Bw. Charles Edward Kichere ambaye ameteuliwa kuwa CAG. Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait. Kabla ya Uteuzi huo, Mhandisi Aisha Amour alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali Francis Ronald Mbindi kuwa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Kanali Francis Ronald Mbindi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Gabriel Pascal Malata ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali (Deputy Solicitor General)
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Majaji 12 wa Mahakama Kuu. Walioteuliwa ni;
Dkt. Zainabu Diwa Mango.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Zainab Diwa Mango alikuwa Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Bw. Edwin Elias Kakolaki.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Edwin Elias Kakolaki alikuwa katika Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya Nchini.
Dkt. Deo John Nangela.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Deo John Nangela alikuwa katika Ofisi ya Tume ya Ushindani (Fair Competition Commission - FCC).
Bw. Fredrick Kapela Manyanda.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Fredrick Kapela Manyanda alikuwa katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Bi. Elizabeth Yoeza Mkwizu.
Kabla ya uteuzi huu Bi. Elizabeth Yoeza Mkwizu alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani.
Augustine Karichuba Rwizile.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Augustine Karichuba Rwizile alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama.
Bw. Ephery Sedekia
Kabla ya uteuzi huu Bw. Ephery Sedekia alikuwa Katibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Attorney General – AG).
No comments:
Post a Comment