TGNP YAWANOA WANAWAKE WANAOOMBA NAFASI ZA UONGOZI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 28 October 2019

TGNP YAWANOA WANAWAKE WANAOOMBA NAFASI ZA UONGOZI


Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Bi. Asseny Muro (katikati) akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake waliotia nia kuingia katika kinyang'anyiro cha nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mtaa. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TNGP Mtandao, Bi. Lilian Liundi pamoja na mwezeshaji, Bi. Agripin Moshi (kulia).

Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Bi. Asseny Muro (wa pili kulia) akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake waliotia nia kuingia katika kinyang'anyiro cha nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mtaa. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TNGP Mtandao, Bi. Lilian Liundi pamoja na mwezeshaji, Bi. Agripin Moshi (kulia).

 Mkurugenzi Mtendaji wa TNGP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (wa pili kulia) akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Bi. Asseny Muro (wa kwanza kulia) kufungua rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake waliotia nia kuingia katika kinyang'anyiro cha nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mtaa. 

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake waliotia nia kuingia katika kinyang'anyiro cha nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mtaa. 

TGNP Mtandao imewakutanisha baadhi ya wanawake waliotia nia kuingia katika kinyang'anyiro cha nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mtaa unaotarajia kufanyika hivi karibuni.

Akizungumza na akinamama hao wakati akifungua mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Bi. Asseng Muro aliwataka kutambua nafasi wanaoziomba ni haki yao hivyo kuwataka wapambane kuzipigania.

Alisema fursa ya uongozi ni haki ya pande zote kiume na kike na imetambuliwa hadi katika mikataba ya kimataifa na kuridhiwa na mataifa anuai. Hivyo wanawake wana haki ya kupewa nafasi za uongozi.

"Mwanamke kuingia katika uongozi kuna thamani ya kipekee, kwani inaaminika kuwa wanawake ni makini pale wanapopata nafasi za uongozi na wengi wamekuwa hawayumbishwi," Bi. Asseng Muro. Aliwataka wanawake watakaofanikiwa kupata uongozi mbali na kubeba ajenda za wanawake pia wanabeba sauti za wasiosikika hivyo kutoa manufaa kwa jamii yote.

Pamoja na hayo aliwashauri akinamama hao kutotumia njia chafu za hongo kuingia madarakani bali kutumia njia sahihi ambayo itawaweka huru katika kutekeleza majukumu yao ya uongozi; 'Uamuzi wa kugombea unaitaji mikakati na ushawishi hivyo kuwataka akinamama hao kutokubali kubweteka bali kupambana kushindania nafasi walizoziomba.'

"...Naomba mtambue kugombea ili ushinde unaitaji mbinu na mikakati, lazima pia ujiamini kushinda," Nendeni mkaibebe ajenda ya wanawake vema na kuhakikisha mnaitetea katika kipindi chote cha uongozi wenu pale mtakapofanikiwa," alisisitiza Bi. Asseng Muro.

Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Bi. Asseny Muro (katikati) akiwaonesha washiriki wa mafunzo hayo (hawapo pichani) nakala ya Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake wanayotakiwa kuibeba.

Mwezeshaji katika semina hiyo, Bi. Hilda Dada (mbele) akiwasilisha mada kwa washiriki.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake waliotia nia kuingia katika kinyang'anyiro cha nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mtaa. 

No comments:

Post a Comment