RC ALLY HAPI ATOA SIKU SABA UJENZI WA SOKO LA MLANDEGE KUKAMILIKA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 24 October 2019

RC ALLY HAPI ATOA SIKU SABA UJENZI WA SOKO LA MLANDEGE KUKAMILIKA

 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari wa mkoa Iringa juu ya hatma ya soko kuu la Mlandege lililopo katika manispaa ya Iringa.

 Mkuu wa Mkoa wa Iringa  Ally Hapi akimsikiliza kwa makini mkandarasi wa soko la kisasa la Mlandege Manispaa ya Iringa.

 Moja ya eneo la soko kuu la kisasa la Mlandege lilopo Manispaa ya Iringa.

NA FREDY MGUNDA, IRINGA

MKUU wa Mkoa wa Iringa  Ally salumu hapi amefanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa soko kuu na la kisasa mlandege mjini Iringa na kuagiza kasi ya ujenzi iongezwe na mkandarasi wa Home Africa Constractions Engineering Ltd anayejenga soko hilo ili hadi kufikia October 31 mwaka huu liwe limekamilika tayari kwa matumizi ya wafanyabiashara.

Katika Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama ya kutembelea na kukagua ujenzi wa soko jipya unaoendelea hivi sasa mjini Iringa Hapi alionesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo huku akitoa agizo la kuhakikisha linakamilika mwishoni mwa mwezi huu Mwaka Huu.

“Ndani ya tarehe 31 mwezi huu kumi taa zote,umaliziaji vitu vyote ya soko hili  viwe vimekamilika,nataka ifikapo mwezi wa 11 tarehe 1 tayari muwe tayari kukabidhi mradi  huu wa kisasa kwa halmashauri   ili iweke utaratibu wa  mzuri wa matumizi   kwa hiyo nawapa siku saba tuu soko hili  liwe imekamirika”alisema hapi.

Aidha Hapi alisema kuwa mradi huo unagharimu shilingi bilioni 3.7 huku akimtaka   mkurugenzi wa halmashauri  ya manispaa ya Iringa  na wataalamu kuhakikisha wanaweka mpangilio mzuri wa watu kupata vibanda na maduka  kwa halali bila manung’uniko na waliokutwa mwanzo ndio wapewe kipaumbele.

Alisema mkoa wa Iringa hauna duka kubwa la kisasa la kuuza bidhaa ,hivyo halmashauri iangalie katika soko hilo eneo wanaloweza kuweka kwajili ya uwekezaji wa duka kubwa litakalokuwa linatoa bidhaa zenye ubora ili kuongeza pato la hamashauri.

“Naomba nitumie fursa hii kuwapongeza sana mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela,mkurugenzi na mkandarasi kwa kazi kubwa mliyoifanya kuhakikisha soko hili linakamili hivi karibuni” alisema Hapi 

Simon s. bahegwa ni mkandarasi wa kampuni ya home Africa constractions alimesema kuwa thamani ya mradi ilikuwa shilingi bilioni 3.72 na ifikapo tarehe 31 october watakuwa wamekamilisha kama alivyoagiza mkuu wa mkoa.

“ mheshimiwa kufikia  tarehe 31 mwezi huu tutakuwa tumekamilisha mradi huu kwa asilimia 100 kwa tukimaanisha kufunga taa ,na thamani ya mradi huu ilikuwa ni shilingi bilioni 3.72 na fedha iliyotumika mpaka sasa ni bilioni 2.6 tunategemea kukabidhi mradi  huu mwishoni mwa mwezi huu”alisema bahegwa

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya iringa HAMID NJOVU alisema kuwa soko hilo la Mlandege linaukubwa wa Squermeter 3182 ambapo wanatarajia likianza kutumika litakuwa likiingiza mapato ya shilingi million 55 mpaka milioni 80 kwa mwezi.

Mradi wa ujenzi wa soko jipya la Mlandege Manispaa ya Iringa  unagharimu taklibani shilingi bilioni 3.7 kwa fedha za serikali unaotarajiwa kuwa na jumla ya  wafanyabiashara 2000 .

No comments:

Post a Comment