NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AKAGUA MIUNDOMBINU MKOANI KIGOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 1 October 2019

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AKAGUA MIUNDOMBINU MKOANI KIGOMA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa (wapili kulia), akifafanua jambo kwa Mbunge wa Kasulu mjini mhe. Daniel Nsanzugwako (wa pili kushoto), alipokagua miundombinu ya uwanja wa ndege na barabara wilayani Kasulu, (kushoto), ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.

Muonekano wa uwanja wa ndege wa Kasulu unaotarajiwa kuboreshwa ili kuruhusu ndege nyingi na kubwa kutua katika uwanja huo na hivyo kuhuisha huduma za usafiri wa anga mkoani Kigoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa ( kulia), akifafanua jambo kwa Mbunge wa Kasulu mjini mhe. Daniel Nsanzugwako (wa pili kulia), alipokagua miundombinu ya uwanja wa ndege na barabara wilayani Kasulu, (kushoto), ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.

Muonekano wa daraja la Kilombero linalojengwa katika barabara ya Kasulu-Kidahwe KM 63, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea mkoani kigoma.

Baadhi ya wananchi wilayani  Kasulu wakitoa pongezi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa na Mbunge wao mhe. Daniel Nsanzugwako kufuatia kasi ya ujenzi wa barabara ya Kasulu-Kidahwe Km 63 kwa kiwango cha lami.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment