DHAMIRA YA SERIKALI NI KUHAKIKISHA MTAMBO WA HALE UNAREJEA KWENYE HALI YA KAWAIDA - WAZIRI KALEMANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 18 October 2019

DHAMIRA YA SERIKALI NI KUHAKIKISHA MTAMBO WA HALE UNAREJEA KWENYE HALI YA KAWAIDA - WAZIRI KALEMANI

 Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani kushoto katikati akionyeshwa kitu ni Mhandisi Mkuu wa Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Pangani Hydro System Jackline Mtolela wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo hicho.

 Mhandisi Mkuu wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Pangani Hydro System Jackline Mtolela  kulia akimuonyesha kitu Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kushoto wakati wa ziara yake kwenye kituo hicho.

Mhandisi Mkuu wa Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Pangani Hydro System Jackline Mtolela  kushoto akiwa na  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia chini ya mgodi wa Hale  wakati wa ziara yake kwenye kituo hicho.

 Sehemu ya mitambo iliyopo kwenye kituo hicho cha kuzalisha umeme.

Meneja wa Tanesco mkoa wa Tanga Julius Sabu kulia akipitia taarifa wakati wa ziara hiyo.

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema serikali itahakikisha mtambo wa kuzalisha umeme wa hale unarejea kwenye hali yake ya kawaida ili uweze kutoa megawatts 21 kama ilivyosanifiwa na kuanza kufanya kazi mwaka 1964.

Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme cha Hale wilayani Korogwe mkoani Tanga ambapo pia alitembelea mgodi wa kufua umeme.

Akiwa kwenye kituo hicho Waziri Kalemani alisema kwamba ametembelea mradi huo kwenye maeneo makubwa mawili ya mashine na trasfoma huku akieleza kwamba kwenye mashine mbili ambazo zipo eneo hilo hazifanyi kazi kwa sasa maanake hatupati megawati hata moja kutoka kwenye mtambo huo.

Alisema kwamba ingawa mtambo mmoja unafanyiwa marekebisho kwa maana ya kufungwa vifaa na wataalamu hivyo watahakikisha unakamilika na tayari alikwisha kutoa maekelezo kazi hiyo ikamilike ili megawatts 10.5 zirejee.

“Hapa katikati mlikuwa mnapata megawatts 8 zilikuwa hazifiki hata kumi ..wakati huu matengenezo makubwa yanafanyika hivyo ni matumaini yake kwamba hata mkandarasi ambaye anatafutwa kwa ajili ya kufanya matengenezo ya mitambo yote miwili utafanyika haraka “Alisema Dkt Kalemani 

Hata hivyo alisema lazima wahakikisha wanakuwa na umeme wa kutosha ambao utapatikana kwenye mradi huo ambao ni wa miaka mingi kwani ulijengwa mwaka 1964 hiyo mitambo kila wakati lazima ifanyiwe ukarabati hasa wakati unapopita.

“Mwaka juzi nilipita hapa na kutoa maekelezo kutokana na kuwepo dalil za mitambo iliyochakaa nikawaambia muanze utaratibu wa kufanya marekebisho ya mitambo yote wakati wa ziara yangu kupita kwenye mitambo ni kujihakikisha umeme unapatikana na wa uhakika.”Alisema.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhandisi Mkuu wa Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Pangani Hydro System Jackline Mtolela alimueleza Waziri Kalemani kwamba hali ya mitambo iliyopo kwnye kituo hicho ni chakavu ya mwaka 1964ina hitaji matengenezo makubwa.

Alisema kutokana na hali hiyo hivi sasa wapo kwenye mchakato wa kupata wakandarasi ili waweze kufanya ukarabati kwani kwa sasa wana uwezo wa kuzalisha megawatts 10.5 kwa mashine moja ila kutokana na uchakavu wa mashine wanazalisha megawatts 8 lakini mashine ipo kwenye matengenezo.

No comments:

Post a Comment