Mgeni Rasmi,
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa
Madini akiwasili Mahafali ya 15 ya Shule ya Sekondari Busangi iliyopo
Halmashauri ya Msalala, Wilaya Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 16, 2019.
Akizungmza kwenye Mahafali hayo, Biteko
alitoa ahadi ya mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya
madarasa shuleni hapo huku akiungwa mkono na viongozi wa Serikali na taasisi
mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala aliyeahidi kupeleka
Tsh. 25,000,000 (milioni 25) kwa ajili ya ujenzi huo.
Aidha Biteko
aliahidi kutoa Tsh. 500,000 (laki tano) kwa kila mwanafunzi atakayefaulu kwa
daraja la kwanza katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne katika Shule hiyo
ya Sekondari Busangi.
Na George Binagi, Mwanza
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko akipungia wananchi mkono alipokuwa akiwasili kwenye Mahafali hayo.
Kijana wa Skauti akimvisha Skafu Mgeni Rasmi, Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko.
Wahitimu wa Shule ya Sekondari Busangi wakiimba wimbo wa kuwaaga wenzao kwenye Mahafali hayo.
Viongozi mbalimbali meza kuu.
Mgeni Rasmi, Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko akizungumza kwenye Mahafali hayo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Busangi akisoma taarifa ya Shule hiyo.
Katibu Tawala Mkoa Shinyanga akitoa salamu za Serikali kwenye Mahafali hayo.
Wahitimu.
Mgeni Rasmi, Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko akikabidhi vyeti kwa wahitimu pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo taaluma.
No comments:
Post a Comment