Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe. |
RAIS wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefariki dunia. Tayari mmoja wa wanafamilia ameithibitishia BBC kuwa, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.
Taarifa zinasema Mugabe alikuwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu kabla ya umauti kumfika.
Mugabe ambaye jina lake lilivuma zaidi ulimwenguni akiwa madarakani kwa muda mrefu, ameiongoza Zimbabwe kutoka 1980 mpaka 2017, alipong'olewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa jeshi.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa tayari amethibitisha kupitia mtandao wa twitter juu ya taarifa za kifo hicho cha mtangulizi wake.
"Kamarada Mugabe alikuwa ni mwanga wa mapinduzi, mwana umajui wa Afrika ambaye aliyatoa maisha yake katika ukombozi na kuwawezesha watu wake. Mchango wake kwa taifa letu na bara (la Afrika) hautasahaulika..." ameandika Mnangagwa.
-BBC
No comments:
Post a Comment