NDEGE YA TANZANIA YAREJEA, YASIMAMISHA SAFARI ZA AFRIKA KUSINI KWA MUDA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 6 September 2019

NDEGE YA TANZANIA YAREJEA, YASIMAMISHA SAFARI ZA AFRIKA KUSINI KWA MUDA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi  Isack Kamwelwe akitoa taarifa ya kurejea kwa ndege ya Tanzania akiwa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.

KIKOSI CHA USHINDI- jopo la wapambanaji waliofanikisha kurejea kwa ndege ya Air Tanzania.

BAADA ya ndege ya Tanzania iliyoshikiliwa nchini Afrika Kusini kwa amri ya mahakama kurejea nchini Tanzania. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi  Isack Kamwelwe ametangaza ndege hiyo kusitisha safari za Afrika Kusini hadi pale hali ya machafuko ya vurugu za kuwashambulia wahamiaji wa kiafrika yatakapotulia.

"...Napenda kuwajulisha kuwa ndege yetu iliyozuiliwa nchini Afrika Kusini imerejea Tanzania, ilitua jana (juzi) usiku majira ya saa moja na kwa sasa tumesimamisha safari za Afrika Kusini kwa muda...lakini wateja wetu wanaoelekea huko wataendelea kupata huduma bila usumbufu. Tumefanya hivyo kwa kuwa tusingependa kuwapeleka abiria sehemu ambayo inavurugu...," alieleza Mhandisi  Isack Kamwelwe katika Ukumbi wa Ubungo Plaza.

Aidha Waziri kamwele aliwapongeza timu ya wanasheria na viongozi waliokuwa nchini Afrika Kusini, wakiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dk. Damas Ndumbaro kwa kushughulikia shauri hilo hadi kufanikisha kuirejesha nyumbani ndege hiyo ya Air Tanzania aina ya Airbus A220-300.

Taarifa zaidi zinasema Jaji wa Mahakama ya Afrika Kusini akisoma hukumu ya shauri hilo, alisisitiza kuwa Afrika Kusini haina mamlaka ya kisheria (jurisdiction) ya kuliamulia jambo hilo.

Ndege hiyo ilikuwa imeshikiliwa katika uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg kwa amri ya mahakama, dhidi ya mkulima Hermanus Steyn aliyefungua kesi kuidai Serikali ya Tanzania.

Naibu Waziri, Ndumbaro alinukuliwa akisema kuwa Serikali ya Tanzania imeshamlipa Steyn dola milioni 20, maana yake wapo tayari kumalizia bakaa ya deni, lakini mkulima huyo "anatakiwa kurudi katika mahakama za Tanzania, na aache kuihusisha Afrika Kusini."

No comments:

Post a Comment