NMB YABORESHA MFUMO WA ULIPAJI KWA KUTUMIA KADI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 30 September 2019

NMB YABORESHA MFUMO WA ULIPAJI KWA KUTUMIA KADI

Waziri wa Habari, Utalii, Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mheshimiwa  Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Maofisa wa Benki ya NMB alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Maonesho ya pili ya 'Zanzibar Tourism Show'  Visiwani Zanzibar.

Maofisa wa Benki ya NMB wakifurahi pamoja na Waziri wa Habari, Utalii, Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mheshimiwa  Mahmoud Thabit Kombo baada ya kukabidhiwa cheti cha shukrani kwa udhamini wao.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (mwenye miwani) akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya pili ya 'Zanzibar Tourism Show' Visiwania Zanzibar.

UONGOZI wa Benki ya NMB umesema kuwa unazidi kuboresha mifumo ya huduma zao za kadi ili kuhamasisha watalii pamoja wananchi wa kawaida kutumia kadi kwenye malipo na ununuzi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Philbert Casmir wakati akizungumza kwenye maonesho ya Utalii visiwani Zanzibar, ambapo benki hiyo ni moja wapo ya mdhamini mkuu wa maonesho hayo yaliyofika tamati siku ya Jumamosi.

Alisema kutokana na ukuaji wa Teknologia Duniani, ndivyo wanavyo buni mbinu zitakazo wawezesha wateja wao kupata huduma bora na za kimataifa. Vilevile, mifumo ya Kidigitali na matumizi ya kadi za MasterCard ambazo zinatumika kitaifa na kimataifa  zimekua zikiondoa usumbufu kwani huduma hizo zinaweza kutumikaa ndani na nje ya nchi.

Benki ya NMB benki hivi sasa ipo karibu na wananchi mjini na vijijiNI  hivyo kuingia katika masauala ya utalii, kwa kiasi kikubwa itasaidia kuzidi kujitangaza na kuvutia wateja wengi zaidi pamoja na wageni wanaofika nchini.

Naye Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar- Balozi Seif Ali Iddi ameomba mashirikiano na taasisi nyingine katika kutangaza utalii wa Zanzibar ili kuongeza idadi kubwa ya watalii Zanzibar.

Alisema wananchi wa Zanzibar wananufaika na utalii kupitia sera ya Utalii kwa wote na kubainisha kuwa sera hiyo ipo wazi  kuweza kunufanisha wananchi hasa kwa kuwa na usalama wa nchi.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale- Mahamoud Thabiti Kombo alisema kuwa maonyesho hayo ni agizo la Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, ambapo lengo ni kuitanganza Zanzibar kiutalii baada ya mafanikio makubwa ya waka jana.

Alisema kuwa maonesho ya kila mwaka yanawasadia wajasiriamali wadogo wadogo kujitangza kupitia utalii ili waweze kunufanika na matunda ya utalii kwa kuuza bidhaa na kukuza biashara zao.

Kwa upande wake Meneja wa NMB tawi la Zanzibar - Abdalla Duchi, amewataka wananchi wa Zanzibar kuchangamkia fursa za utalii zinazopatika  nchini ili kujikwamua na umaskini .

Amewataka wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati  kutumia fursa zinazotolewa na Benki hiyo katika maeneo mbalimbali kwa kujisajili kuwa mawakala, ambapo itafungua fursa za ajira sambamba na kutoa huduma kwa wananchi wa kawaida ikiwemo watalii wanaokuja kutembea Zanzibar.

Aliongeza kuwa benki ya NMB ina wateja zaidi ya milioni tatu huku ikiongoza kwa matawi mengi - 229 nchini, yakiwemo NMB Zanzibar, NMB Mwanakwerekwe na NMB Chakechake- Pemba, huku ikiwa na jumla ya mawakala 84 Zanzibar kwa jumla ya idadi ya  mawakala 6000 nchi nzima.

No comments:

Post a Comment