MATUKIO KATIKA PICHA VIJANA MKOANI GEITA WAKIPATIWA ELIMU YA UJASIRIAMALI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 22 August 2019

MATUKIO KATIKA PICHA VIJANA MKOANI GEITA WAKIPATIWA ELIMU YA UJASIRIAMALI

Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Silas Daudi akitoa mada kuhusu Mpango wa Biashara kwa vijana wanajihusisha na shughuli mbalimbali za biashara na ujasiriamali katika Mkoa wa Geita ikiwa ni awamu ya tatu ya Mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 yanayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Baadhi ya Wajasiriamali wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mmoja ya watoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Julius Tweneshe akielezea mada kuhusu taratibu za kufungua kampuni wakati wa mafunzo hayo.

Sehemu ya wajasirimali kutoka Mkoa wa Geita wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Mmoja wa vijana kutoka Kiwanda cha Chaki cha Rubondo akielezea jambo kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo katika upatikanaji wa masoko.

Baadhi ya Wajasiriamali walioshiriki kwenye mafunzo hayo wakijadiliana kazi kwenye vikundi.


No comments:

Post a Comment