WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YATWAA TUZO MBILI MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 13 July 2019

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YATWAA TUZO MBILI MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA

Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wapili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, tuzo ya mshindi wa pili miongoni mwa mabanda bora ya Wizara, Idara na Taasisi za serikali.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango na  Msemaji wa Wizara hiyo Bw. Benny Mwaipaja, akionesha moja kati ya tuzo mbili ambazo Wizara imenyakua kwenye maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa (DITF), Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakifurahia tuzo mbili ambazo Wizara imepata katika Maonesho hayo.

Na Mwandishi Wetu, WFM, Dar es Salaam

WIZARA ya Fedha na Mipango, imetwaa tuzo mbili kwa mpigo kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayofikia kilele Jumamosi Julai 13, 2019.

Katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonesho hayo kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa (Ceremonial dome) , Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alikabidhi tuzo hizo moja baada ya nyingine, kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja.

Akizungumzia tuzo hizo Bw. Mwaipaja alisema moja ni ya mshindi wa pili katika ubunifu wa mfumo wa ukusanyaji maduhuli ya serikali (GePG) ambao umerahisisha mfumo wa malipo kwa wananchi, wakiwemo pia wafanyabiashara, na wawekezaji.

Aidha, Taasisi mbili za Wizara ya Fedha na Mipango, ikiwemo Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), zimetwaa tuzo ya mshindi wa Tatu katika utoaji wa Elimu bora ya Juu na Usimamizi makini wa wataalamu wa Ununuzi na Ugavi.

Maonesho hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere maarufu Sabasaba, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, yamebeba kauli mbiu isemayo "Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda."

No comments:

Post a Comment