WANACHAMA
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) popote pale walipo
Tanzania bara na Visiwani, wamesogezewa huduma karibu ambapo Mfuko una jumla ya
ofisi 29 mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.
Meneja
wa Mfuko huo Mkoa wa Temeke, Bi. Ritha Ngalo, amewaambia waandishi wa habari
kwenye banda la PSSSF namba 13 kwenye viwanja vya Maonesho ya 43 ya biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam Julai 10, 2019 kuwa kwa wale watakaofanikiwa
kufika kwenye Maonesho hayo, yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba jijini
Dar es Salaam, wasisite kupita kwenye banda hilo ili wapatiwe huduma sawa na
zile wanazohitaji kuzipata kwenye ofisi mbalimbali za Mfuko.
Serikali
kupitia Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma namba 2 ya
mwaka 2018 ilifuta mifuko ya hifadhi ya jamii ya PPF, PSPF, LAPF na GEPF na kuanzisha Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii kwa Waatumishi wa Umma PSSSF.
Maonesho
hayo yanatarjiwa kufikia kilele Julai 13, 2019.
Mstaafu Francis
Ramadhan Njau, (kulia), ambaye alikuwa Afisa Ushirika Daraja la I, akihudumiwa na Meneja
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mkoa wa Temeke, Bi.Ritha
Ngalo kwenye banda la Mfuko kwenye viwanja vya Maonesho Sabasaba jijini
Dar es Salaam Julai 10, 2019. Aliyesimama kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi
wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi.
Wanachama wa PSSSF, wakiwa tayari wamehudumiwa.
Mwanachama akipatiwa taarifa alizohitaji kutoka PSSSF alipotembelea banda la Mfuko huo Julai 10, 2019.
![]() |
Afisa Michango PSSSF Bi. Getrude Athanas (kulia), akimpatia maelezo ya kina mwanachama huyu aliyetembelea banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. |
Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Donald P. Maeda (kulia), akihakikisha kila swali alilokuwa nalo Mwanachama huyu linapatiwa majibu kwa vielelezo.
Meneja
wa Mfuko huo Mkoa wa Temeke, Bi. Ritha Ngalo, (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Mfuko huo Julai 10, 2019. Kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfukmo huo Bw. Abdul Njaidi.
No comments:
Post a Comment