DK KIJAJI AAHIDI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI IHARI...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 10 July 2019

DK KIJAJI AAHIDI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI IHARI...!


Na Mwandishi Wetu, Kondoa, Dodoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dk. Ashatu Kijaji (Mb) ameahidi kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ardhi katika Kijiji cha Ihari wilayani Kondoa, baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoishi katika Kijiji hicho.

Ahadi hiyo aliitoa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji hicho ambapo wananchi na viongozi walipata nafasi ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Wananchi wa Kijiji hicho walieleza kuwa mgogoro huo umesababisha wengi wao kukosa mahala pa kuchungia mifugo yao kwa kuwa eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya malisho limevamiwa na kubadilishwa matumizi kuwa mashamba.

Dkt. Kijaji ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini, alisema taarifa za mgogoro huo ataziwasilisha kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ili aweze kutatua changamoto hiyo ambayo imekuwa kero kwa wananchi hao.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mheshiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni Serikali ya wanyonge na imepanga kutatua kero mbalimbali za wananchi ikiwemo migogoro yote ya ardhi nchini.

Dkt. Kijaji aliwaomba wananchi hao wawe na Subira katika kipindi hiki ambacho Serikali inaenda kushughulikia tatizo lao huku akibainisha kuwa utatuzi wa mgogoro huo unategemea sana utulivu wao kama walengwa.

“Niwaombe ndugu zangu tueendelee kuilinda amani ya Ihari, tuendelee kuilinda amani ya Kondoa na nchi yetu kwa ujumla katika kipindi hiki ambacho tunamsuburi Waziri wa Ardhi ambaye anajua matumizi ya kila kipande cha ardhi nchini, atatue mgogoro huu”, alisisitiza.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihari, Bw. Idi Lumba amemshukuru Dkt. Kijaji kwa kutenga muda wa kusikiliza changamoto zao hususan tatizo la ardhi ambalo lilianza kuwagawa wananchi wake.

Bw. Lumba alimhakikishia Mbunge huyo kuwa hali ya Kijiji cha Ihari itaendelea kuwa tulivu kwa kipindi chote ambacho watakuwa wanasubiria suluhu ya mgogoro huo, huku akielezea changamoto ya maji na umeme katika Kijiji hicho ambazo Dkt. Kijaji aliahidi kuzitatua kwa haraka.

“Imani yetu ni kwamba maelekezo na elimu ambayo tumeitoa naamini wachimbaji wadogo wakiifanyia kazi sisi tupo tayari kuwakopesha tulikuwa tunashindwa kutokana na namna ambavyo walikuwa wakihama hama lakini naamini maelekezo tuliyowapa watayatekeleza,” Alisema Filbert.

Baadhi ya wachimbaji wadogo Mkoani humo,wameishukuru Benki ya NMB kuwa tayari kuwakopesha kwenye shughuli zao na kwamba kupitia mikopo ambayo watapatiwa itawasaidia kwa kiasi kuboresha shughuli zao za uchimbaji ambazo wamekuwa wakizifanya kila siku.



Mbunge wa Kondoa Vijijini ambae pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihari, Busi, wilayani Kondoa, ambapo wananchi hao walilalamikia tatizo la mgogoro wa ardhi, linalowasumbua kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment