|
Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuelezea namna Benki ya NMB ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud. |
|
Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuelezea namna Benki ya NMB ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud. |
|
Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuelezea namna Benki ya NMB ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd akiwa katika mkutano huo. |
|
Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuelezea namna Benki ya NMB ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd akiwa katika mkutano na wanahabari. |
|
Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuelezea namna Benki ya NMB ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB, Vicent Mnyanyika akiwa katika mkutano huo. |
|
Mmoja wa wateja wa Benki ya NMB (kushoto) akipata huduma ndani ya Banda la Benki ya NMB alipotembelea banda hilo. |
BENKI ya NMB imejipanga kutoa huduma zote za kibenki wa washiriki na wananchi wanaotembelea maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari leo ndani ya Banda la Benki ya NMB, Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd alisema benki hiyo imejipanga kutoa huduma zote muhimu za kibenki ili kuhakikisha wanakidhi mahitaji yote kwa washiriki wa maonesho hayo.
Aliwataka washiriki na wananchi wengine kutoumiza vichwa pindi watakapo hitaji huduma za kibendi ndani ya viwanja hivyo kwani benki hiyo imejipanga kutoa huduma zote muhimu za kibenki.
Aidha aliwaomba wananchi kutembelea Banda la NMB kujipatia huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata maelezo ya huduma mpya na bora kwa wateja wake.
Kwa upande wake Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya viwanja vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud aliongeza kuwa huduma za NMB ndani ya maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa ni sawa na huduma zinazotolewa na tawi lolote kubwa la NMB hivyo kuwashauri wananchi kutembelea kipata huduma zote muhimu ndani ya viwanja hivyo.
"...Huduma za NMB zinazotolewa katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere ni sawa na huduma zinazotolewa na tawi letu lolote...tuna mambo mengi mazuri kwa wateja na watakaotutembelea waje kwa wingi wafurahiye huduma zetu," alisema Bi. Masoud.
No comments:
Post a Comment