WAZAZI WATUMIA ZAIDI YA MILIONI 70 KUKARABATI SHULE YA MSINGI MAPINDUZI ENGLISH MEDIUM - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 19 June 2019

WAZAZI WATUMIA ZAIDI YA MILIONI 70 KUKARABATI SHULE YA MSINGI MAPINDUZI ENGLISH MEDIUM

 Mwenyekiti wa shule ya msingi Mapinduzi English medium Haliel Abdallah akionyesha jinsi gani ukarabati wa madarasa na ofisi sita za walimu za shule hiyo kwa lengo la kuboresha miundombinu ya shule hiyo.

 Mafundi wakiwa kazini kuendelea na ukarabati wa majengo ya shule hiyo ya msingi Mapinduzi English medium iliyopo manispaa ya Iringa. 

Mwenyekiti wa shule ya msingi Mapinduzi English medium Haliel Abdallah akiwa na kiongozi mwingine kwenye kama hiyo wakikagua ukarabati ambao unaendelea.

NA FREDY MGUNDA, IRINGA

WAZAZI wa shule ya msingi Mapinduzi English medium iliyopo manispaa ya Iringa wameamua kuikarabati ili kuboresha mazingira ya shule kwa lengo la kukuza taaluma ya wanafunzi katika shule hiyo.

Akizungumza na blog hii Mwenyekiti wa shule hiyo, Haliel Abdallah alisema kuwa shule hiyo ilikuwa na miundombinu mibovu ambayo ilikuwa sio rafiki kwa walimu na wanafunzi hivyo ilikuwa inachangia kutoingia kwenye shule nyingine za aina hiyo.

“Kwa kifupi sana kamati ilibaini kwamba mazingira ya madarasa pamoja na ofisi za walimu hazikuwa rafiki hivyo tukaamua kuanza kufanya tathimini kwa lengo la kuanza kukarabati shule hiyo ili irudi kwenye ubora kama uliokuwepo hapo awali,” alisema Abdallah.

Abdallah alisema kuwa lengo la kujenga darasa jipya katika shule hiyo ili kupanua wigo wa kuwa na vyumba vingi ambavyo vitatuasaidia kuleta ushindani na shule nyingine zenye mchepuo wa masomo ambayo yanafundishwa kwa lugha ya kingereza.

“Tunataka kuhakikisha kuwa shule hii inakuwa kwenye ubora wa hali ya juu kwenye miondombinu kuanzia madarasa,ofisi za walimu na mazingira ya shule lazima yawe ya kuvutiwa kwa walimu,wanafunzi na hata wazazi wawe wanajisifia watoto wao kusoma katika shule hiyo,” alisema Abdallah

Abdallah aliongeza kwa kusema kuwa katika ukarabati huo utahusisha pia ukarabati wa madawati pamoja kuhakikisha walimu wanakuwa na samani  bora ambazo nazo zinakuwa rafiki na mazingira ya kufundishia na kuandalia masomo.

Aidha Abdallah amewapongeza wazazi ambao watoto wao wanasoma katika shule hiyo kwa kujitoa kukakikisha shule hiyo inakarabatiwa kwa lengo la kuwa nashule yenye kushindana na shule nyingine zilizopo mkoani Iringa na nje ya Iringa.

Awali akitoa taarifa ya hali ilivyokuwa hapo awali walimu mkuu wa shule hiyo Emanuel Mwakyusa alisema kuwa miundombinu ya shule hiyo haikuwa rafiki kwa kutoa elimu iliyobora kwa kuwa madarasa na majengo mengi yalikuwa chakavu sana.

“Madarasa mengi yakuwa chakavu hivyo ikawa ngumu kufanya usafi kukiwa na mashimo, paa zilikuwa zimechoka na kuvujisha maji kipindi cha vua hiyo hali ya usafi ilikuwa mbaya na kusababisha kutoa elimu ambayo ilikuwa haistahili,” alisema Mwakyusa

Mwakyusaalisema kuwa ukarabati huo umefanywa na wazazi tu bila kuigusa serikali kwa kuwa wazazi hao wanapenda kufanya maendeleo kwa lengo la kuhakikisha waoto wao wanasoma katika mazingira yaliyo bora.

“Mimi niwapongeze wazazi ambao watoto wao wanasoma katika shule hii kwa kujitoa kwa moyo wao wote kuhakikisha kuwa shule hii inakarabatiwa vilivyo na kuwa na mazingira yaliyo bora,” alisema Mwakyusa.

Mwakyusa alisema kuwa ukarabati huo utasaidia kukuza taaluma za wanafunzi wa shule hiyo kwa kuwa miundombinu itakuwa imeboreshwa vilivyo na itakuwa rafiki wa pande zote
Kwa upande wake mwalimu Rahab Mahenge alisema uboresha wa miundombinu ya shule hiyo kutachangia kuongezeka kwa ufaulu kwa kuwa watu wote watakuwa na furaha na mazingira yaliyopo.

No comments:

Post a Comment