TAASISI YA KIRAIA YA AQUA-FARMS YAADHIMISHA SIKU YA BAHARI DUNIANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 10 June 2019

TAASISI YA KIRAIA YA AQUA-FARMS YAADHIMISHA SIKU YA BAHARI DUNIANI

Mkurugenzi wa Aqua-Farms Organization Bw. Jerry Mang'ena akitoa neno la ufunguzi wakati wa kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani lililofanyika BUNI Hub jijini Dar es Salaam, ambapo maadhimisho hayo hufanyika kila ifikapo Juni 8 kila mwaka.

Mhe. Sware Semesi (MB), (aliyesimama)  akitoa salamu wakati wa kongamano maalum la Siku ya Bahari Duniani lililoandaliwa na Aqua-Farms Organization  ambapo alisisitiza sera bora ni muhimu katika kuhakikisha kuna Malengo Endelevu katika kutunza na kulinda Bahari.

Bw. Kervin Robert Kutoka UNESCO Tanzania,akisoma ujumbe kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO  Bi. Audrey Azoulay kwa ajili ya Siku ya Bahari Duniani, alisema wanawake wanahusika sana katika maswala ya Bahari kwa malengo endelevu.

Afisa Mawasiliano wa Aqua-Farms Organization Bi. Nancy Iraba akisisitiza baadhi ya mambo muhimu kuhusiana na siku ya Bahari Duniani.

Dr Rosie Marie Mwaipopo akielezea mambo mbalimbali yanayohusiana na utunzaji wa Bahari na kusisitiza kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na utamaduni wa kulinda na kutunza Bahari kwa maendeleo endelevu.


Katibu Mkuu wa Youngship Tanzania Bw. Gregory Mella Akitoa mada fupi kuhusiana na maswala ya Bahari  akihusisha na maswala ya jinsia wakati wa Siku mdaharo wa siku ya Bahari Duniani.


Majadiliano yakiendelea.

Mkurugenzi wa Aqua-Farms Organization Bw. Jerry Mang'ena akitoa neno la Shukurani baada ya kumaliza kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali kuzungumzia maswala ya Bahari.

 Picha ya Pamoja baada ya Kongamano hilo muhimu la maswala ya bahari kukamilika.

No comments:

Post a Comment