WAZIRI MKUU DK MWIGULU AZINDUWA MKUTANO MKUU WA 19 WA WAKAGUZI WA NDANI, IIA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 22 September 2026

WAZIRI MKUU DK MWIGULU AZINDUWA MKUTANO MKUU WA 19 WA WAKAGUZI WA NDANI, IIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanziber, Dk. Saada Mkuya Salum (katikati) akikabidhiwa zawadi na Rais wa Chama cha Wakaguzi wa Ndani (IIA), Bw. Jonathan Ngoma (kulia) mara baada ya kumuwakilisha Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye hafla ya uzinduzi rasmia wa Jukwaa maalumu la 13 la Utawala Bora linalofanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 19 wa Wakaguzi wa Ndani (IIA) Jijini Arusha.



Rais wa Chama cha Wakaguzi wa Ndani (IIA), Bw. Jonathan Ngoma (kulia) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmia wa Jukwaa maalumu la 13 la Utawala Bora linalofanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 19 wa Wakaguzi wa Ndani (IIA) Jijini Arusha.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanziber, Dk. Saada Mkuya Salum akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmia wa Jukwaa maalumu la 13 la Utawala Bora linalofanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 19 wa Wakaguzi wa Ndani (IIA) Jijini Arusha, ambapo alimwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania Dk. Mwigulu.

Rais wa Chama cha Wakaguzi wa Ndani (IIA), Bw. Jonathan Ngoma (kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanziber, Dk. Saada Mkuya Salum kwenye hafla ya uzinduzi rasmia wa Jukwaa maalumu la 13 la Utawala Bora linalofanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 19 wa Wakaguzi wa Ndani (IIA) Jijini Arusha.



Na Mwandishi Wetu, Arusha

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amezinduwa rasmia Jukwaa maalumu la 13 la Utawala Bora linalofanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 19 wa Wakaguzi wa Ndani (IIA) Jijini Arusha.

Akisoma Hotuba ya Waziri Mkuu, Dk. Saada Mkuya Salum, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanziber kwa niaba ya Dk. Mwigulu amesema mkutano huo ni muhimu kwa ajili ya utoaji huduma ikiwa ni sambamba na kukabiliana na mabadiliko chanya katika kuzijenga taasisi ili kufikia malengo kwa pamoja kwa kuzingatia matumizi ya mifumo na teknolojia.

Alisema Serikali itaendelea kushirikiana na wakaguzi wa ndani kwa kuboresha nyenzo katika utendaji kazi yao kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji, sheria, kanuni, miongozo na utawala bora ikiwa ni mkakati wa kufikia malengo yenye tija kwa taasisi za umma na binafsi.

Katika hotuba hiyo ya Waziri Mkuu, Dk. Nchemba, amesema mikutano ya namna hiyo ni muhimu kwa ajili ya utoaji huduma, ikiwa ni sambamba na kukabiliana na mabadiliko chanya katika kuzijenga taasisi ili kufikia malengo kwa pamoja kwa kuzingatia matumizi ya mifumo na teknolojia.

“Ukaguzi wenye thamani ni ule unao tolewa na kufanyiwa kazi kwa taasisi husika katika kuboresha utendaji kazi na kufikia malengo yaliyo kusudiwa, kwani maendeleo hayategemei uwekezaji pekee bali rasilimali watu na Fedha katika miradi ya kimkakati hivyo ipo haja kufanya kazi kwa kizingatia sheria na kitambua fursa za maboresho ya kimfumo,” alisema Dk. Mwigulu katika hotuba hiyo.

Kando na hilo katika hatua nyingine, Waziri Dk. Saada akatumia jukwaa hilo kutoa maelekezo ya Serikali kwa Chama cha Wakaguzi wa Ndani (IIA), ikiwa ni pamoja na kuwataka wataalamu wa kada hiyo kufanya kazi kwa uhuru, kukubali mabadiliko kwa kuzingatia utawala bora na ubunifu.

“Ukaguzi wenye thamani ni ule unao tolewa na kufanyiwa kazi kwa taasisi husika katika kuboresha utendaji kazi na kufikia malengo yaliyo kusudiwa,” alisema Dk. Saada.

Awali katika salamu zake kwa wajumbe, viongozi wa taasisi za Serikali na sekta binafsi kupitia jukwaa hilo, Rais wa Chama cha Wakaguzi wa Ndani (IIA), Bw. Jonathan Ngoma anesema kwa muda mrefu wakaguzi wa ndani wamekuwa wakifanya kazi zao kwa kuzingatia uhuru.

Aidha amebainisha kuwa jukwaa hilo linalenga kubadilishana uzoefu kwa wataalamu, kujifunza kwa wataalamu wa ndani na kimatifa hasa katika kukabiliana na viatarishi pamoja na matumizi ya teknolojia ikiwemo matumizi ya akili unde.

Jukwaa hilo maalumu la 13 la utawala Bora linalo enda sambamba na mkutano Mkuu wa 19 kwa wakaguzi wa ndani (IIA) unaoendelea jijini Arusha.

Rais wa (IIA) ameweka wazi kuwa licha ya uwepo wa fursa kadhaa kupitia mkutano huo, bado wataalamu wa kada hiyo kumekuwa wakipitia changamoto, ikiwemo kupishana kwa sheria za ndani na mifumo ya kimataifa ya kazi za ukaguzi wa ndani na kutolea mfano wa namna bora ya kuripoti baadhi ya taarifa za ukaguzi kwa bodi ambayo ni sehemu ya walio kaguliwa.

“Mfano tunategemea mkaguzi wa ndani au idara ya ukaguzi wa ndani iweze kuripoti kwa bodi husika ya taasisi, lakini wakati mwingine bodi ile ni sehemu ya walio fanyiwa ukaguzi ndani ya taasisi,” alisema Rais wa IIA.

Naye, Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Laurent Luswetula ametumia fursa hiyo kueleza namna Serikali inavyo endelea kuboresha michakato ya upatikanaji wa sheria kwa ajili ya wakaguzi wa ndani jambo ambalo linatajwa kuongeza tija zaidi kwa uchumi wa nchi na miradi ya kimkakati kwenye taasisi za Serikali.

Jukwaa hilo limewakutanisha wanachama hai wataalamu wa ukaguzi, na viongozi wa Serikali zaidi ya elfu moja ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ikiwa ni nisehemu ya kuelekea mkutano mkuu wa 19 wa taasisi ya wakaguzi wa ndani (IIA) na kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC Jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment