Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi. |
Na Christopher Philemon, Monica Mutoni, Geneva-Uswisi
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dk. Agnes Kijazi yupo nchini Uswisi – Geneva kwenye Mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-18 Congress). Mkutano huu hufanyika kila baada ya miaka 4 ambapo mwaka huu unafanyika jijiji Geneva kuanzia tarehe 3- 14 juni, 2019.
Katika Mkutano huo utafanyika uchaguzi wa viongozi wakuu wa WMO, ambao ni pamoja na Rais Makamu wa Kwanza wa Rais, Makamu wa Pili wa Rai, Makamu wa Tatu wa Rais na viongozi wengine wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).
Tanzania kupitia Dk. Agnes Kijazi amejitosa katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya makamu wa tatu wa Rais wa WMO. Dk. Kijazi anaungwa mkono na wakuu wote wa taasis za hali ya hewa barani Afrika na azimio hili lilipitishwa katika Mkutano wa Mawaziri wenye Dhamana ya Huduma ya Hali ya Hewa Barani Afrika (African Ministerial Conference on Meterology - AMCOMET) tarehe 18 - 23 Februari, 2019 Jijiji Cairo Misri ambapo Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye ambaye kupitia hotuba yake alifanikiwa kuwaombea wajumbe kumpitisha Dk. Kijazi kama mgombea pekee barani Afrika.
“Kutokana na umuhimu wa nafasi tunayoiomba kwa Taifa na Afrika kwa ujumla, na hasa ukizingatia heshima ambayo tumepewa na Nchi za Afrika kuweka azimio la kumuunga mkono Dk. Kijazi, ili achaguliwe katika nafasi ya makamu wa tatu wa rais ambayo ina wagombea wengine kutoka mabara mengine, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Kushirikiana Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,zinazendelea kushiriki katika kuomba wajumbe kutoka nchi mbalimbali hapa mjini Geneva kumpigia kura Dk. Kijazi ili ashinde nafasi hiyo,” alisema Nditiye.
Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iliandaa hafla ya kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania kwa kuwaalika wajumbe mbalimbali wa mkutano wa 18 wa WMO. Aidha katika salamu za viongozi wakuu wa WMO akiwepo Rais wa sasa wa WMO, Bw. David Grimes aliwaomba wajumbe kumuunga mkono Dk. Kijazi kutokana na uchapa kazi wake, kauli ambayo ilirudiwa pia na Katibu Mkuu wa WMO Prof. Petteri Telaas alisema pamoja na utendaji uliotukuka wa Dk. Kijazi, bado shirika hilo halijawahi kupata kiongozi kike kwenye nafasi ya juu kama hiyo hivyo akawaomba pia wamuunge mkono.
No comments:
Post a Comment