MWILI WA DK. MENGI WAWASILI KILIMANJARO, VILIO, MAYOWE VYATAWALA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Wednesday 8 May 2019

MWILI WA DK. MENGI WAWASILI KILIMANJARO, VILIO, MAYOWE VYATAWALA

Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi ukiwasili mkoani Kilimanjaro ukitokea Dar es Salaam na kuelekea nyumbani kwa marehemu Machame.

Na Mwandishi Wetu, Machame

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi umewasili mkoani Kilimanjaro ukitokea Dar es Salaam na kuelekea moja kwa moja nyumbani kwa marehemu Machame.

Mwili huo uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA na kuanza msafara kuelekea Machame ambapo njiani ulilakiwa na wananchi mbalimbali wakiwa wameshika majani kuashiria kuomboleza kifo cha Dk. Mengi kuwagusa waombolezaji.

Magari ya msafara wa mwili wa Dk. Mengi yakiongozwa na askari wa Jeshi la Polisi yalilazimika kusimama na pengine kupunguza mwendo baada ya wananchi kufunga njia wakitaka kutoa ishara ya kwa heri kwa kiongozi huyo aliye kusa jamii.

Vilio na mayowe vilisikika kila yalipokuwa maeneo ya makundi ya waombolezaji wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kumsubiri njiani kutoa ishara ya kumuaga kwa kumpungia mkono lilipopita gari lililobeba mwili wa Dk. Mengi.

Wengine walisikika wakilia na kupunga matawi ya majani ikiwa ni kuoneshwa kuguswa na msiba huo wa Dk. Mengi kipenzi cha watu hasa wenye ulemavu na makundi mengine.

Magari ya polisi yakiwa na askari katika msafara huo yalionekana kupata changamoto baadhi ya maeneo baada ya kukumbana na makundi ya waombolezaji barabarani wengine wakifunga barabara ilimradi kufanikiwa kuona jeneza la mwili wa Dk. Mengi, ambapo asikari walilazimika kushuka kwenye magari na kuwaondoa wananchi polepole ili msafara uendelee kuelekea nyumbani kwake.

Mwili wa marehemu Dk. Mengi kesho unatarajiwa kuagwa katika Kanisa la KKKT Moshi mjini kabla ya kusafirishwa kuelekea Machame tena kwenye makaburi ya familia kwa mazishi.

No comments:

Post a Comment