BENKI YA NMB YAFUTURISHA WATEJA WAKE TANGA, WAOMBA ATM ZAIDI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 20 May 2019

BENKI YA NMB YAFUTURISHA WATEJA WAKE TANGA, WAOMBA ATM ZAIDI

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Omari Mtiga akizungumza na wateja wa Benki ya NMB kwnenye hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo juzi.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Omari Mtiga akizungumza na wateja wa Benki ya NMB kwnenye hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo juzi.

Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Tanga - Juma Luwuchu akizungumza kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort kwa ajili ya wateja wao wa Tanga.

Washiriki wakimsikiliza Shehe Mkuu wa Mkoa wa Tanga akitoa neno la mwezi mtukufu kwenye futari ya NMB. 

Washiriki wakimsikiliza Shehe Mkuu wa Mkoa wa Tanga akitoa neno la mwezi mtukufu kwenye futari ya NMB. 

Na Mwanandishi Wetu, Tanga


BENKI ya NMB imeombwa kuangalia uwezekano wakuongeza matawi ya vituo vya kutolea fedha ATM ili kuhakikisha inasogeza huduma zake za kibenki karibu na wananchi katika Jiji la Tanga.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Meya wa Jiji la Tanga Alhaj  Mustapha Selebosi hapo jana wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.

Alisema kuwa kutokana na Jiji la Tanga kukuwa kiuchumi benki hiyo inatarajia kuongeza matawi ya ATM katika maeneo ya Amboni pamoja na Pongwe ili wananchi wa maeneo hayo waweze kufurahia huduma za kibenki.

“Tunawashukuru benki hii kwa kuona umuhimu wa kuandaa futari kwa ajili ya wateja wake ili kuweza kuwakutanisha pamoja na kuweza kuwatambua kwa lengo la kukuza umoja na mshikamano,”alisema Meya huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya wateja binafsi kutoka NMB makao makuu Omari Mtiga alisema kuwa wamefarijika kama benki kuwa sehemu ya kutoa sadaka ya futari hiyo kama sehemu ya kuunga mkono waumini wa dini ya Kiislamu nchini. Alisema kuwa ni utaratibu wa benki hiyo kila mwaka kushiriki katika futari mbalimbali kwa lengo la kuomba dua pamoja na na kuomba yaliyo mema na wateja wao.

“Tunathamini jumuiya ya Waislamu katika kipindi hiki na tumelenga kuhakikisha shughuli hii inafika kwenye  kanda zote nchi nzima hivyo naamini kwa kupitia sadaka hiyo mungu atawajalia kheri na Baraka,” alisema Mtiga.

Kwa upande wake Shekhe wa mkoa wa Tanga Juma Luwuchu aliwataka waislamu kuhakikisha wanadumisha yale mema na mazuri yaliyoelekezwa katika kitabu cha mwenyezi mungu.

“Kutoa mchango kwa ajili ya mambo ya dini ni jambo la Baraka kwani mafundisho ya dini yanatuelekeza Baraka zipo nyingi kwenye kutoa sadaka hivyo tujitahidi kutoa ili tupata Baraka,” alisema Shekhe Luwuchu.

No comments:

Post a Comment