NMB YACHANGIA MABATI 802, MADAWATI 50 NA VITANDA 8 VYA HOSPITALINI MKOA WA RUKWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 1 April 2019

NMB YACHANGIA MABATI 802, MADAWATI 50 NA VITANDA 8 VYA HOSPITALINI MKOA WA RUKWA

Naibu Waziri Tamisemi Mh Josephat Kandege akizungumza jambo mara baada ya kukabidhiwa Msaada wa Mabati 802, Vitanda 8 vya Hospitali pamoja na Madawati 50 vyenye Jumla ya Thamani ya shilingi Mil 35 Kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ,Straton Chilongola Mwenye Suti nyeusi (kulia) hafla ambayo imefanyika katika Soko la Wakulima Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.March 30,2019.

Naibu Waziri Tamisemi Mh Josephat Kandege akizungumza jambo mara baada ya kukabidhiwa Msaada wa Mabati 802, Vitanda 8 vya Hospitali pamoja na Madawati 50 vyenye Jumla ya Thamani ya shilingi Mil 35 Kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ,Straton Chilongola Mwenye Suti nyeusi (kulia) hafla ambayo imefanyika katika Soko la Wakulima Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.March 30,2019.

Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Straton Chilongola (Kulia) akimkabidhi Madawati 50 Naibu Waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege (MB) kwa ajili ya Chuo cha Veta Kalambo Mkoani Rukwa, Kushoto Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangambo, Vitu vingine vilivyotolewa na Benki hiyo ya NMB kwa ajili ya Chuo hicho ni pamoja na Vitanda 8 vya hospitali, Mabati 802, hafla ambayo imefanyika katika Soko la wakulima Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Marchi.

BENKI ya NMB imechangia jumla ya mabati  802 kwa ajili ya kuezeka madarasa ya Chuo cha Veta Kalambo, Shule za Kipeta na Ilanga pia kuzipa madawati 50, pamoja na Vitanda 8 vya Hospitali vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 35.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Straton Chilongola alisema benki hiyo imekuwa ikiguswa na changamoto za sekta ya elimu nchini na mara zote imeipa kipaumbele kwa kutambua kwamba elimu ni uti wa mgongo wa taifa.

Alisema Benki ya NMB inatambua juhudi za Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ya kusimamia elimu kwa nguvu zote, pamoja na kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari hivyo ina kila sababu kuunga mkono.

"...Sisi kama wadau ambao Serikali inamiliki hisa asilimia 32, tunawajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo kupitia kusaidia jamii kwani ni kupitia jamii hii hii, ndo imetufanya benki ya NMB kuwa hapa ilipo kubwa kuliko benki yoyote hapa nchini," alisema.

Aidha alibainisha kuwa NMB imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Mkoa mzima wa Rukwa hasa katika kuchangia maendeleo ya jamii, kwani kwa mwaka 2017/18 pekee imetumia zaidi ya shilingi milioni 80 kusadia elimu na afya.

Aliyataja baadhi ya maeneo yalionufaika na msaada huo ni shule anuai na vituo vya afya vya Mtowisa, Mfinga, Msila, Kasesera, Kirando na Namanyere, huku shule zilizonufaika ni pamoja na Chanji, Laela,Nkasi, Mfinga na Mkangale.

Hata hivyo, NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita zaidi kwenye miradi ya elimu (Madawati, vifaa vya kuezeka), afya (Vitanda na magodoro yake) na kusaidia majanga yanayoipata nchi yetu. Tunatambua kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wetu wengi wanapotoka, kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni wetu.

No comments:

Post a Comment