Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata amewataka wanafunzi wa manispaa ya Iringa kujifunza uzalendo kuwa na uzalendo wa nchi yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo inayosaidia kuleta maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikivuruga amani. |
Mwenyekiti wa umoja wa vijana Manispaa ya Iringa (UVCCM) Salvatory Ngerera aliwataka wanafunzi kuwa makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio chanzo cha kuharibu maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na uzalendo wan chi yao. |
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiongea na wanafunzi walijitokeza kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya mwembetogwa. |
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
NAIBU MEYA wa manispaa ya
Iringa amewataka Wanafunzi wa Manispaa ya Iringa kujifunza uzalendo kuwa na
uzalendo wa nchi yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo
inayosaidia kuleta maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi
vimekuwa vikivuruga amani.
Akizungumza na baadhi ya
wanafunzi wa Shule ya Mwembetogwa, Lugalo, Tagamenda na Mawelewele naibu meya Joseph Lyata aliwataka wanafunzi
hao kujifunza nini maana ya kuwa mzalendo na ndio silaha pekee ya kuhakikisha
tunakwepa kuanzisha vita kwenye nchi hii.
"Kuthamini vitu vilivyopo katika
nchi yako ni moja ya kuwa mtanzania mzalendo kwa kuwa utakuwa unalinda mali za
nchi na kuhakikisha amani inakuwepo kwa kuna wananchi ambao ni wazalendo na
nchi yao bila kujali itikadi ya vyama vilivyopo katika nchi hiyo,” alisema Lyata
Lyata alisaema kuwa nchi nyingi
ambazo hazijaingia kwenye vita ni nchi zile ambazo zimekuwa zikibadilishana
uongozi bila kutumia mabavu, hivyo utaona nchi nyingi zinapigana kwa ajili ya
kugombea madaraka lakini hali tofauti kwa nchi ya Tanzania.
“Angalieni nchi kama Somalia tu
hapo jirani wanavyopigana kwa ajili ya kugombea kuongoza nchi huo sio uzalendo
wa wananchi wa Somalia ndio maana leo hii nawaambieni kuwa lazima mjifunze nini
maana ya uzalendo ili kulinda na kuthamini amani ya nchi yenu,” alisema Lyata.
Lyata aliongeza kwa kusema kuwa
uzalendo kwa wananchi wa Tanzania umeanza kupungua kwa kuwa watu wengi hawajui
nini maana ya kuwa mazalendo hivyo wanatakiwa kujifunza katika umri huo kuwa
wazalendo na nchi yao.
“Lazima tuambizane ukweli
kabisa maana sisi kama manispaa tunahakikisha manispaa inaendelea kuongoza
kwenye usafi,kuhakikisha wanafunzi mnasoma vizuri bila kuwa na woga na
kuhakikisha tunailinda mipaka ya nchi yetu huo ndio uzalendo wa nchi yetu,”
alisema Lyata.
Lyata aliwata wanafunzi kuanza
kuwa na uzalendo kuanzia pale ulipozaliwa au ulipokulia ndio utaanza kuijenda
nchi hii kwa kuwa umeenza kuthamini toka ulipokuwa mdogo hadi ukubwani kwa kuwa
watakuwa na lengo la kulinda amani ya nchi.
“Uzalendo pia huanzia pale
unapohuzulia mikutano ya hadhara kwa lengo la kujifunza na kujua muelekeo wa
mtaani kwako au kujua mwelekeo wa taifa kwa kuwa kwenye kila mkutano wa hadhara
kuna mambo ya msingi utajifunza tu” alisema Lyata.
Naye mwenyekiti wa umoja wa
vijana manispaa ya Iringa (UVCCM) Salvatory Ngerera aliwataka wanafunzi kuwa
makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio chanzo cha kuharibu
maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na uzalendo wan chi yao.
“Wananchi wanasababisha
umasikini wenyewe kutokana na kuchagua viongozi ambao hawana uwezo ndio
hupelekea umaskini katika kwa wananchi
waliomchagua kiongozi waliyekuwa na imani naye, hivyo kukosea kuchagua kiongozi
bora ni kujitafutia matatizo wenyewe,” alisema Ngerera.
Ngerera aliongeza kwa kuwaambia
wanafunzi hao kuwa sehemu ya kumfundisha wananchi uzalendo ni katika umri huo
waliona wanafunzi kwa kuwa ndio kipendi ambacho wengi wameanza kuwa na uelewa
wa maisha ni nini.
“Jamani lazima mjifunze
mnapotaka kumlaumu kiongozi mlimchagua wenyewe ni lazima mjipie wenyewe kwanza
mlikosea wapi na sasa mnatakiwa mfanye nini ili kuhakikisha mfanya kazi huku
mkiwa mmetawaliwa na uzalendo wenu” alisema Ngerera.
No comments:
Post a Comment