Baadhi ya washiriki waliofika katika kikao hicho cha utoaji tuzo kwa utunzaji bora wa mazingira na kuwa na vyoo bora. |
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa sambamba na Mkurugeni wa Halmashauri ya Iringa vijijini Robert Masunya wakinywa maziwa ya ASAS. |
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
MKUU wa Wilaya ya Iringa
Richard Kasesela amewataka viongozi wa sekta ya afya katika Halmauri ya Iringa
vijijini kuendelea kutundika bendera nyekundu kwa wananchi ambao hawana vyoo
bora ili kutumisha usafi na afya kwa wananchi wote.
Akizungumza wakati wa utoaji
tuzo kwa wananchi,viongozi,taasisi na jumuiya mbalimbali kwa kutekeleza vizuri
kampeni ya kuwa na vyoo bora ambavyo vimeipa ushindi Halmasahuri ya Iringa
Vijijini kwa kupata tuzo ya usafi hapa nchini.
Kasesela alisema kuwa ofisi ya
afya katika halmasahuri ya Iringa Vijijini wamekuwa wakisimamia vizuri swala la
afya na kuwa na vyoo bora ambapo wanataraji kuwa halmashauri ya kwanza kwa kuwa
na vyoo bora kuliko halmashuri zote za mkoa wa Iringa hadi taifa.
“Nampengeza bibi afya wa hapa
amekuwa mkali kuhakikisha hakuna mtu anayeweza kukwamisha zoezi lolote la
kuboresha sekta ya afya na kuhakikisha afya za wananchi wa wilaya hii wanakuwa na
afya njema” alisema Kasesela
Aidha Kasesela amepiga marufuku
wa wazazi kujifungulia majumbani kwa kuwa sio sehemu salama kwa uzazi wa mtoto
wakati serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya ambayo ndio kipaumbele cha
serikali ya awamu ya tano.
“Jukumu la kwanza kwa baba ni
kuhakikisha amempeleka mama kliniki kupata huduma ili kuwa na malezi mazuri ya
mtoto,hivyo tutaondoa ile njia ya akinamama kujifungulia majumbani kwa kuwa
tayari baba atakuwa anajua wajibu wake” alisema Kasesela
Kasesela amewataka watendaji wa
kata,vijiji na maafisa tarafa kuhakikisha hakuna mama anajifungulia nyumbani na
nitamshughulikia mtendaji yeyeto Yule ambaye hata wachukulia hatua akibaba
watakao fanikisha mama kujifungulia numbani.
Awali akitoa hutuba kwa mgeni
rasmi mkurugenzi wa halmasahuri ya Iringa Vijijini Robert Masunya aliwataka watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha
wameendeleza juhudi hiyo ya kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na vyoo bora ili
kupunguza na kumaliza tatizo la milipuko ya magonjwa.
“Niwaombeni tena tuendelee kushirikiana
vyema katika kuhakikisha halmasahuri ya Iringa Vijijini inaongoza kwa kuwa na
mazingira bora na safi kuliko halmashuri zote hapa nchini kwa kuwa tuna
mikakati ambayo ni bora sana” alisema Masunya
No comments:
Post a Comment