Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad. |
MAHOJIANO YA CAG NA TBC LEO...!
CAG; Hili linaweza kuwa tatizo kubwa zaidi badala ya kuwa solution. Kwa hiyo mimi nafikiri, tukae chini tutazame halafu tuone athari ni zipi ili kuepuka matatizo tunayoweza kuyasababisha. Lakini naamini mimi kuna watu wenye busara na probably wanatoa busara zao, wasiwasi wangu ni kwamba huenda likawa tatizo kubwa zaidi kuliko ambavyo linaonekana sasa hivi..
TBC; kwanini unaamini hivyo? Kwamba huenda likawa ni tatizo kubwa zaidi tofauti na linavyoonekana sasa?
CAG; Kwa sababu technically tunaweza kuwa na 'constitutional crises' kwamba, report (taarifa) zishawasilishwa kwa Rais na mimi siwasilishi 'report' bungeni. Kwa hiyo Rais atasababisha taarifa zile ziende bungeni katika siku sita zijazo na kama bunge likikataa kupokea hilo ni tatizo kubwa zaidi. Ni 'contempt' hiyo. Kwa hiyo wasiwasi wangu ni huo. Na zikashawasilishwa bungeni zinakuwa 'public documents' na mimi napata fursa ya kuzungumza na hilo pia linaweza kuwa tatizo kwa hiyo tafsiri ya "hatutafanya kazi na CAG" ni tafairi pana sana inatakiwa tuijue vizuri. Sasa kama nilivyokueleza mwanzo, mimi sijapata hizi habari kwa uhakika, nitazitafuta leo nitaongea na watu wangu na tutajua halafu tutafanya na tathmini ni kitu gani tunaweza kufanya labda..
TBC; unafikiri labda unaweza kuchukua maamuzi magumu kufuatia hatua hiyo ya bunge?
CAG; Mimi sina maamuzi yoyote ya kuchukua bwana. Mimi nachokifanya (mara nyingi hapa) ni kufanya DUA tu basi. Kwamba watu waongoze vizuri na wafanye maamuzi ambayo yana faida na nchi hii basi. Lakini mimi sina kitu cha kufanya. Nina 'constitutional details' zangu nitaendelea nazo na nitaendelea kuzitekeleza.
TBC; katika kile ambacho uliitiwa kwenye kamati ya bunge ambayo wengi hatufahamu na wewe ndie unaefahamu, unafikiri unajutia wakati mwingine ukitafakari kuhusu kile ulichokuwa umesema katika moja ya chombo cha habari huko nje kama ulivyoambiwa kwamba 'umedhalilisha bunge kwamba bunge ni dhaifu?
CAG; mazungumzo haya yote yalifanyika katika kamati na majibu yalitolewa katika kamati na RAI yangu ni kuwa tafuta -hansard- ya kamati na ukiipata utaona maswali yalikuwa yapi na majibu yetu yalikuwa ni yapi bwana..
TBC; CAG tukushuru sana kwa muda wako, haswa kwa ushirikiano wako katika mazungumzo haya.
No comments:
Post a Comment