Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiongea na wanafunzi na viongozi wa chuo kikuu cha Iringa waliokuwa kwenye mkesha wa kuabudu na kuomba na kuwataka waamini wote kujiandaa kabla hawajaanza kusali ili kuweza kuyafikisha maombi yao vilivyo kwa mwenyezi mungu. |
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na moja ya kwaya iliyota burudani siku hiyo ya mkesha wa kuabudu na kuomba. |
Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuku cha Iringa wakiwa kwenye mkesha huo. |
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
MKUU wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amewataka waamini wote kujiandaa kabla hawajaanza kusali ili
kuweza kuyafikisha maombi yao vilivyo kwa mwenyezi Mungu.
Akizungumza wakatika wa
mkesha na kuabudu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa mkoani Iringa Kasesela
alisema kuwa kila jambo ambalo unatarajia kulifanya ni lazima ujiandae
kwanza.
“Mimi katika maisha yangu
kabla sijafanya jambo huwa natafuta muda wa kulifikiria jambo hilo ndio
nalifanyia kazi ndio maana mara nyingi nimekuwa na maamuzi sahihi katika
kufanya kazi zangu kila wakati,” alisema Kasesela.
Kasesela aliwataka wanafunzi
hao kufanya maombi ya kukiombea chuo hicho ili kuendelea kuwa chuo bora hapa
nchini na nje ya nchi na kuendelea kuutangaza mkoa wa Iringa kwa kuwa jina la
chuo hicho limebeba jina la mkoa wa Iringa.
“Chuo hiki kilitaka kufungwa
kwa ajili ya mambo ambayo hayana miguu wa kichwa hivyo naowaomba mkiombee chuo
hiki ili kisije kikafungwa au kufikiriwa kufungwa tena maana kimekuwa kikitoa
elimu iliyo bora sana” alisema Kasesela
Aidh Kasesela alisema
kwanini kanisa la KKKT limekuwa kanisa ambalo limegawanyika katika kanda
mbalimbali ambapo kila ukanda unafanya mambo bila kuwa na ushirikiano wowote
ule na dayosisi nyingine.
“Ukiangalia maisha ya
viongozi wanaofanya kwenye kanda mbalimbali wanatofautiana kuanzia mishahara na
maisha yao yamekuwa yanatofauti kubwa sana
sasa nawaomba leo hii mliombee pia hili ili kanisa liwe na umoja” alisema
Kasesela.
Kasesela alisema kuwa
mgawanyiko huo utasabisha vyou vingi vya KKKT kufa kutokana na kutokuwa na
ushirikiano kama ilivyokuwa na vyuo vingine hapa.
Kwa upande wake Askofu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gavile aliwataka
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa kukesha na kukiombea chuo mara kwa mara.
Ombeni nanyi mtapewa kwa
kuwa mnaomba kwa nia njemba na Mungu nimoto ambao unaweza kuwabariki kila mmoja
wetu hapa hivyo nawaomba tena kuendelea kuomba,” alisema Askofu Gavile
Askofu Gavile alimushukuru
na kumpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa utendaji wake wa
kazi kwa wananchi wote kwa kuwa anaitendea haki nafasi hiyo anayoteuliwa na
Rais.
No comments:
Post a Comment