RAIS MAGUFULI AMPA MCHEZAJI WA ZAWANI TAIFA STARS, PETER TINO MILIONI 5 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 25 March 2019

RAIS MAGUFULI AMPA MCHEZAJI WA ZAWANI TAIFA STARS, PETER TINO MILIONI 5

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mchezaji wa zamani wa  Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Peter Tino ambaye alifunga goli moja lililoipeleka Tanzania kwa mara ya kwanza katika michuano ya AFCON mwaka 1980 iliyofanyika nchini Nigeria. Pia Rais Dkt. Magufuli amemsaidia mchezaji huyo wa zamani kiasi cha Shilingi milioni tano. 

Peter Tino (kulia) akisaini mara baada ya kukabidhiwa fedha kiasi cha shilingi milioni 5 zilizoingizwa Benki ya CRDB, fedha hizo amepewa na Rais Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Peter Tino (kushoto) akikabidhiwa kadi ya CRDB baada ya kuwekewa fedha alizopewa na Rais Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

MCHEZAJI wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino amekabidhiwa shilingi Milioni 5 alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambayo ilifuzu kuingia robo fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON).

Peter Tino ndiye aliyefunga goli lililoiwezesha Tanzania kuingia robo fainali na tangu mwaka 1980 Tanzania haikufanikiwa kuingia hatua hiyo mpaka mwaka 2019 ikiwa ni miaka 39 imepita.

Peter Tino amealikwa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 25 Machi, 2019 wakati Mhe. Rais Magufuli alipokutana na kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambao jana waliifunga Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) na kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika baadaye mwezi Juni 2019 huko Misri.

Pamoja na kupatiwa shilingi Milioni 5, Peter Tino ameunganishwa katika zawadi ya kupatiwa kiwanja Jijini Dodoma kwa kila mchezaji wa Taifa Stars iliyotolewa na Mhe. Rais Magufuli ambapo naye atapatiwa kiwanja cha kujenga nyumba. Fedha za Peter Tino zimewekwa katika akaunti yake ya Benki ya CRDB na kukabidhiwa kadi yenye taarifa zake za benki (ATM).


Bondia wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo kutoka Tanga akizungumza mara baada ya kupewa nafasi Ikulu jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment