Na Khalfan Said
KAMATI
ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, imeridhishwa na mabadiliko
makubwa ya kiutendaji ndani ya Shirika la Umeme Nchini TANESCO, ambapo ndani ya
kipindi kifupi limeondokana na utegemezi wa ruzuku ya serikali na sasa linajiendesha lenyewe.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dk. Raphael M. Chegeni wakati wa
hitimisho la ziara ya Kamati kwenye mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme
utokanao na gesi asilia, Kinyerezi 1 (Kinyerezi I Extension) jijini Dar es
Salaam, leo Machi 18, 2019.
“TANESCO
ni Shirika ambalo limekumbwa na changamoto nyingi miaka ya nyuma, lakini tumefurahi kuona
kwamba baadhi ya mambo yaliyokuwa mazito sana mmefanikiwa kuyatatua na hii ni
dalili njema ni nzuri sana kwa sababu sasa hata serikali yetu ya awamu ya tano
toka imeingia madarakani, TANESCO badala ya kuwa mtegemezi mkuu wa ruzuku ya
serikali, hivi sasa Shirika halitegemei tena ruzuku ya serikali hili ni jambo
jema sana.” Alisema.
Mmetoka
kwenye ruzuku na sasa mnakua mnajitegemea haya ni mafanikio endeleeni kupunguza
gharama, na mpanue wigo wa watumiaji wa umeme, watanzania wanahitaji umeme wenye gharama nafuu na haya ndio malengo ya serikali ya awamu ya tano, alisema Dk. Chegeni na kuongeza.
Mpango
wa Serikali wa kujenga umeme wa maji kule Rufiji ni mpango sahihi kabisa na
watanzania wote wazalendo lazima tuunge mkono juhudi hizo kwa sababu tunahitaji
umeme ambao ni wa gharama ya chini ili umeme
umfikie kila mtanzania kwa gharama nafuu.
Aidha
Mwenyekiti huyo ameahidi kuwa Kamati yake itaiomba serikali kupitia Ofisi ya
Msajili wa Hazina iangalie namna gani madeni yanayoikabili TANESCO kwa miaka
mingi yanaondolewa ili iweze kujiendesha kikamilifu na kwa ufanisi zaidi.
“Madeni
ambayo TANESCO inadaiwa huko nyuma Serikali iyabebe.” Alisisitiza. Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO, Mhandisi Dk. Alexander
Kyaruzi ameiambia Kamati hiyo kuwa Kituo cha kuzalisha umeme wa gesi asilia cha
Kinyerezi I kina uwezo wa kutoa Megawati 150 kwa sasa na upanuzi unaoendelea
hivi sasa utaongeza Megawati 185 na hivyo mradi utakapokamilika mwezi Agosti
mwaka huu wa 2019, Kinyerezi I na I Extension itakuwa na jumla ya Megawati 335,
huku Kinyeerzi II ambayo imekamilika ina uwezo wa kuzalisha Megawati 240 za
umeme.
“Kinyerezi
itakuwa complex kubwa sana ya
kuzalisha umeme, tutaendelea na ujenzi wa Kinyerezi III na Kinyerezi IV.”
Alifafanua.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka alisema
Shirika limejiwekea mikakati endelevu ili kuhakikisha linaendelea kutoa huduma
bora kwa wananchi ambapo baada ya kudhibiti deni ambalo Shirika limekuwa
likidaiwa kwa muda mrefu, sasa wameanza kuwalipa wadai wa Shirika sambamba na
kuondokana na kutegemea ruzuku ya kutoka serikalini.
"Kwa takriban miezi minane iliyopita deni ambalo TANSECO tumekuwa tukidaiwa limepungua kwa asilimia 3 naweza kusema limedhibitiwa." Alisema na kuomba sasa ni vema kama Serikali ingelichukua hilo deni au kututafutia mkopo ili tulimalize deni hilo kwani hii itapunguza uwezekano wa kuongezeka kutokana na interest maana tunashindana na deni lenyewe." Alifafanua Dkt. Mwinuka.
Alisema Kwa mwaka TANESCO ilikuwa ikipatiwa ruzuku ya serikali kati ya shilingi Bilioni 449 na bilioni 6 kwa mwaka, lakini hiyo sasa ni historia kwani Shirika linajiendesha lenyewe na kwa mwaka huu wa fedha tuna...project Shirika litatengeneza faida ya Shilingi Bilioni 9.
Aidha
Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Lightnes Mauki
amesema, kwa sasa TANESCO imeanza kulipa madeni na tangu Mwezi wa Februari
mwaka huu 2019 wamelipa bilioni 38.7 na ni hatua nzuri na wamekuwa wakitupatia
nakala za malipo kila mwezi wanapolipa.” Alisema Lightnes.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakipatiwa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakipatiwa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
Mjumbe wa Kamati Mhe. Charles Mwijage, akizungumza.
Mbunge wa Kasulu Vijijini Mhe.Vuma Augustine ni miongozi mwa wajumbe waliotembelea mradi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka akizungumza.
Dkt. Mwinuka akimkaribisha Mbunge wa Karatu, Mhe. Willy Qambalo huku Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Dkt. Kyaruzi akishuhudia, wakati wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwkwzaji wa Mitaji ya Umma (PIC).
No comments:
Post a Comment