TTCL YAPEWA MWEZI MMOJA KUONGEZA UPATIKANAJI WA BIDHAA ZAKE VIJIJINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 14 February 2019

TTCL YAPEWA MWEZI MMOJA KUONGEZA UPATIKANAJI WA BIDHAA ZAKE VIJIJINI

Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (Sekta ya Mawasiliano) akizungumza jambo na Menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation alipotembelea shirika hilo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Sekta ya Mawasiliano Dk. Jim Yonaz na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omary Nundu (kulia).

Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati mbele) anayesimamia sekta ya Mawasiliano akisisitiza jambo kwa  Menejimenti ya Shirikisho la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation (hawapo pichani) alipotembelea shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (Sekta ya Mawasiliano) akizungumza jambo na Menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation alipotembelea shirika hilo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Sekta ya Mawasiliano Dk. Jim Yonaz na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omary Nundu (kulia).

Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye anayesimamia Sekta ya Mawasiliano (mbele kushoto) pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation wakitoka kutembelea miundombinu ya mkongo wa taifa wa mawasiliano unaosimamiwa na Shirika la TTCL.

Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye anayesimamia Sekta ya Mawasiliano (mbele kushoto) pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation wakitoka kutembelea miundombinu ya mkongo wa taifa wa mawasiliano unaosimamiwa na Shirika la TTCL. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Sekta ya Mawasiliano, Dk. Jim Yonaz, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omary Nundu na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega wakiongozana na naibu waziri. 


NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye(Mb) amelitaka Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation kuongeza juhudi katika kusambaza Huduma za Mawasiliano ili kuwafikia Wananchi wote katika pembe zote za Nchi,

Akizungumza na Menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL katika ziara yake ya siku moja kukagua utekelezaji wa majukumu ya Shirika hilo, Mhe Nditiye amesema, Serikali inathamini mchango mkubwa wa Shirika hilo na inataka kuona jitihada zaidi zikichukuliwa katika kuboresha ufanisi wa Shirika na Sekta ya Mawasiliano Nchini.

“TTCL ni Shirika la Umma, Nawapongeza kwa yote mazuri mnayoyafanya na hasa kwa ubunifu wa huduma  na gharama nafuu za huduma hizo kwa Wananchi, Huduma ya Video Conference imetoa matokeo mazuri sana, itaokoa muda na gharama kwa kuwawezesha Watendaji wa Serikali kuwasiliana bila kusafiri kutoka eneo moja kwenda jingine. Napongeza pia huduma ya malipo kwa kadi inayotarajia kuanza hivi karibuni, hizi ni juhudi ambazo Serikali inaziunga mkono.”

Pamoja na kupongeza juhudi za TTCL zilizowezesha Shirika hilo kuongeza mapato, idadi ya Wateja wake na wigo wa upatikanaji wa huduma Nchi nzima, Mhe Nditiye ametoa Siku 30 kwa Menejimenti ya Shirika hilo kuhakikisha kuwa linaondoa kero ya upatikanaji wa Vocha na Laini za simu(Simcards) katika maeneo mbalimbali Nchini.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Corporation Mhandisi Omari Nundu amesema, baada ya kufanya vyema katika mwaka 2018, TTCL imejipanga vyema kufanikisha malengo yake kwa mwaka 2019 ambapo limekusudia kuimarisha Idara na Vitengo vyake ili kuongeza viwango vya ubora wa huduma kwa Wateja sambamba na kutekeleza majukumu ya Shirika kwa Umma.

“Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kwa mwaka unaoishia Desemba 2018 inaonesha TTCL kuwa Shirika linalokuwa kwa kasi na kuongeza idadi ya Wateja na wigo wa huduma zake huku huduma za T PESA nazo zikistawi kwa kasi kubwa. Hadi kufikia Januari mwaka huu, T PESA ina Wateja zaidi ya laki tatu, Mawakala elfu kumi na moja na miamala ya takribani Tsh bilioni nne. Nikuhakikishie Mhe  Naibu Waziri kwamba mwaka huu 2019 tutapata mafanikio zaidi kwa kuwa tuna mikakati thabiti itakayotupa matokeo mazuri”, amesema Mwenyekiti Nundu.

No comments:

Post a Comment