Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akikagua moja ya miradi inayojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) kwa kushirikiana na Vikosi vya Ujenzi na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akikagua moja ya miradi inayojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) kwa kushirikiana na Vikosi vya Ujenzi na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akisisitiza jambo kwa wataalamu wa Ujenzi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Sekta yake mjini Dodoma.
Akizungumza na wataalam wa Wakala wa Majengo nchini (TBA), Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) na Vikosi vya Ujenzi vya Wizara hiyo mjini Dodoma Arch. Mwakalinga, amesema ushirikiano huo ukifanikiwa
utawezesha taasisi hizo kubadilishana uzoefu na utaalam katika kujenga na
kusimamia miradi mingi mikubwa kwa
haraka na viwango bora na hivyo kuiongezea serikali mapato.
“Kuanzisa sasa
hakikisheni nyinyi TANROADS,TEMESA ,TBA,na
VIKOSI vya UJENZI mnakutana mara kwa mara ili kujadiliana kwa pamoja na kupeana
uzoefu utakaowezesha miradi ya ujenzi mnayoijenga na kuisimamia inakuwa na
ushirikishwaji wa kitaalam na kiuzoefu ili kuwa na ubora na kuiwezesha
kukamilika kwa wakati ”, amesema Arch. Mwakalinga.
Naye, Mkadiriaji
Majenzi wa Wizara ya Ujenzi QS. Optatus Kanyesi, amemhakikishia Katibu Mkuu
Mwakalinga kuwa ataratibu umoja huo wa Taasisi za sekta za ujenzi ili taasisi
hizo ziwe na uwiano katika ubora wa huduma zake na kuleta tija kwa Serikali na jamii
kwa ujumla.
Katibu Mkuu Mwakalinga,
alikuwa katika ukaguzi wa miradi inayojengwa na kusimamiwa na taasisi zilizo
chini ya sekta ya ujenzi ili kubaini changamoto na mahitaji ya miradi hiyo
mjini Dodoma.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA
MAWASILIANO 14/2/2019
No comments:
Post a Comment