WATEJA 20 NMB WAJISHINDIA 100,000 KILA MMOJA ZA MASTABATA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 21 December 2018

WATEJA 20 NMB WAJISHINDIA 100,000 KILA MMOJA ZA MASTABATA

Meneja Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala (katikati) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Droo ya kwanza ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Kushoto ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Umuddy Hussein akisimamia droo hiyo.

Meneja Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala (katikati) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Droo ya kwanza ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Kushoto ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Umuddy Hussein akisimamia droo hiyo.

Baadhi ya wanahabari na wafanyakazi wa Benki hiyo wakifuatilia tukio hilo Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.

DROO
ya kwanza ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', imefanyika huku wateja 20 wakijinyakulia shilingi 100,000/- kila mmoja.

Washindi hao 20 wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo hiyo ya kwanza ya wateja waliobahatika baada ya kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo huo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass'.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye droo hiyo, Meneja Huduma za Kadi NMB, Bw. Stephen Jilala alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass'.

Droo hiyo ya kwanza iliyosimamiwa na Ofisa Mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Umuddy Hussein iliendeshwa kwa wazi huku wateja wakipigiwa simu na Bw. Jilala kutaarifiwa ushindi wao na kujinyakulia kitita hicho cha fedha.

Akifafanua mara baada ya kuwataja washindi aliwataka wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea.

Alisema takribani wateja 200 wa NMB ambao watafanya malipo kwa mfumo wa 'NMB Mastercard au 'NMB Masterpass' watakuwa kwenye uwezekano wa kujishindia zawadi za fedha, simu janja za kisasa 'Samsung S9+' na mwisho washindi wengine 3 kati yao wawili kujishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai iliyolipiwa kila kitu.

No comments:

Post a Comment