VODACOM YAWATUNUKU WATUMIAJI MTANDAO BOMBA POINTI ZA TUZO ZENYE THAMANI YA BILIONI 1 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 11 December 2018

VODACOM YAWATUNUKU WATUMIAJI MTANDAO BOMBA POINTI ZA TUZO ZENYE THAMANI YA BILIONI 1

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani)  jijini Dar es Salaam juu ya kuwatunuku watumiaji wa mtandao wa Vodacom, points za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1 katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu Noel na Mwaka Mpya” yenye kauli mbiu Nabaki mulemule na Vodacom. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo Rossalyn Mworia.

Kaimu Mkurugenzi wa biashara, Bi. Linda  Riwa (kulia) akifafanua jambo katika mkutano huo na wanahabari. 

VODACOM Tanzania PLC, kampuni ya simu nambari moja nchini, inagonga kengele za shangwe katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunukia wateja wake pointi za Tuzo zenye thamani ya Shilingi bilioni 1 kama sehemu ya mpango wa kampuni kuwashukuru wateja wao.
Programu hii ni ya kwanza kabisa iliyoletwa na kumpuni hiyo ambayo inawapatia wateja wake pinti za tuzo kila waongezapo salio au kufanya miamala ya M-Pesa. Wateja wanaweza kutumia pointi hizo kwa kuzibadili kupitia waleti zao za M-Pesa, kununua bando, na pia kwa kununua bidhaa mbalimbali katika maduka ya Vodacom.
“Mapato ya Vodacom Tanzania yaliongezeka kwa asilimia 6 katika mwaka huu, na ukuaji huu umechangiwa sana na wateja wetu. Hivyo Pointi za Tuzo ni njia ya kuonyesha shukrani zetu kwa watumiaji wetu na kwa moyo wa kutoa, tumeamua kufanya jambo la ziada katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunuku wateja wetu Pointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1,” alisema Hisham Hendi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji.
“Ninawahimiza wateja wetu kuishi maisha ya ki-Tuzo, kununua muda wa maongezi na kufanya miamala mingi kadri inavyowezekana katika M-Pesa hasa katika kipindi hiki cha sikukuu na kujipatia pointi hapo hapo kila wafanyapo miamala hiyo,” aliongeza Hisham.
Wateja hao wanatunukiwa Pointi za Tuzo 50 kwa kila Shilingi 500 wanayotumia kununua salio. Pointi hizi za Tuzo zinaweza kulimbikizwa hadi miezi 12 tangu mtu aanze kujikusanyia na baada ya miezi hiyo 12 zisipotumiwa muda wake huisha. Wateja wa Vodacom wanaweza pia “Kulipa kwa Pointi” moja kwa moja kwa wafanyabiashara wanaopokea M-Pesa, kwa kupiga *149*01#>TUZO>TUZO POINTS>Vuna Pointi> (Nunua bando/Lipa/Badili kwa M-Pesa).

“Mwaka mzima, wateja wetu wamekuwa ndiyo walengwa na kiini cha ubunifu wetu – Vodacom Tanzania tumedhamiri kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora kabisa,” alimalizia Hisham.

Mkurugenzi  wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC hiyo Rossalyn Mworia, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam,(hawapo pichani) juu ya kuwatunuku watumiaji wa mtandao wa Vodacom, points za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1 katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu Noel na Mwaka Mpya” yenye kauli mbiu “Nabaki mulemule na Vodacom.”  Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi   na  Kaimu Mkurugenzi wa biashara Linda  Riwa.

Sehemu ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo. 

No comments:

Post a Comment